Dr Slaa Afungukia Ukweli kwa Jeshi la Polisi Kuhusu Mlinzi wake Kutaka Kumuua

Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Willbroad Slaa, ameripoti katika Kituo cha Polisi Central kilichopo Posta jijini Dar kuhusiana na sakata zima la mlinzi wake anayetuhumiwa kutaka kumuua.
Akizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo, Slaa alisema yeye hakuitwa na Jeshi la Polisi kujielezea bali kutokana na maneno yanavyozidi kusambaa na kuwasilishwa isivyo ameona aende kueleza ukweli ulivyo.
Alisema kuwa, kwa mujibu wa chama chake, ameona ni vyema kwenda kulieleza Jeshi la Polisi kuhusiana na mkasa mzima unaomkabili mlinzi wake, ambapo alikutana na Kamanda wa Kanda Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Suleimani Kova na kumueleza kila kitu kwa kuandika karatasi tisa (9) zenye maelezo yake, hivyo zoezi zima la kutoa taarifa kuhusiana na alichoandika ameliachia Jeshi la Polisi baada ya wao kufanya kazi yao ya Uchunguzi.


“Ndugu zangu waandishi sijaitwa hapa kwa ajili ya mahojiano kama taarifa zinavyozaga lakini kutokana na uongozi nilionao nimeona ni vyema suala hili nilifikishe Polisi na katika maelezo yangu nimeweza kuandika zaidi ya karatasi tisa (9) zenye ukweli hivyo nimeikabidhi kwa Jeshi la Polisi na baada ya wao kufanya uchunguzi watatoa taarifa kamili juu ya kile nilicho kiandika,’’ alisema Dr. Slaa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment