Tido Mhando: Studio Mpya za Azam TV Unaweza Ukazifananisha na za CNN, Aljazeera, BBC, Ujenzi Umegharimu Bilioni 56

Uzinduzi wa studio mpya za kisasa za Azam TV zilizoko eneo la Tabata Relini, jijini Dar es salaam unafanyika leo.

Tido aliendelea, “Azam TV imeanza kufanya shughuli zake kwa zaidi ya mwaka sasa, lakini tumekuwa tukiboresha mambo kadha wa kadha kuelekea siku ya kesho (leo) ambayo tunaweza tukasema ndiyo mwanzo rasmi wa Azam Tv.” Rais Kikwete anatarajiwa kuzindua studio hizo leo March 6.

Studio mpya za Azam TV “Ni studio ambazo labda unaweza ukazifananisha na kampuni kubwa kama CNN, Aljazeera, BBC, na kwakuwa za kwetu ni mpya zinaweza kuwa na ubora kuliko hizo,” alisema Tido.

  Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando ambao ndio wamiliki wa Azam TV, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa studio hizo zimegharimu zaidi ya bilioni 56.
Picha na Bin Zubery
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment