Ushindani wa magwiji wa soka wanaoitikisa dunia kwa sasa Lionel Andrés "Leo" Messi Cuccittini pamoja na Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro, umeendelea kudhihiri baada ya jarida la michezo huko nchini Ufaransa kutoa orodha ya wachezaji wanaoingiza fedha nyingi kwa mwaka.
Orodha iliyochapishwa katika jarida la France Football, inaonyesha wawili hao walioshindanishwa katika kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka 2013 na 2014 wameachana, ambapo mshambuliaji wa FC Barcelona Lionel Messi ndiye kinara anayeingiza fedha nyingi kwa mwaka mzima.
Jarida hilo limeeleza kwamba sifa za wachezaji walioingizwa kwenye orodha hiyo zinazingatia mapato yanayotokana na mishahara pamoja na matangazo ya kibiasha ambayo yamekua yakifanywa na makampuni mbali mbali duniani kote.
Messi yupo kileleni kwa kuingiza kiasi cha paund million 48.1 ambazo ni sawa na EURO MILLION 65 akifuatiwa na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara mbili mfululizo Cristiano Ronaldo, ambaye kwa mwaka mzima ameingiza kiasi cha paund million 40 ambazo ni sawa na EURO MILLION 54.
Katika nafasi ya tatu yupo mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu ya Barcelona Neymar ambaye ameingiza kiasi cha paund million 27.01 ambazo ni sawa na Euro million 36.5 akifuatiwa na mwenzake kutoka nchini Brazil beki wa klabu bingwa nchini Ufaransa PSG Thiago Silva iliyeingiza kiasi cha paund million 20.4 ambazo ni sawa na Euro million 27.5 kwa mwaka.
5. Robin van Persie £18.8m
6. Gareth Bale £17.5m
7. Wayne Rooney £16.5m
8. Zlatan Ibrahimovic £15.8m
9. Sergio Aguero £15.6m
10. Robert Lewandowski £14.8m
Jarida hilo pia limetoa orodha ya mameneja wanaoongoza kwa kuingiza fedha nyingi kwa mwaka kutokana na mishahara wanayolipwa pamoja na matangazo ya biashara wanayofanya na makampuni mbali mbali duniani kote.
1. Jose Mourinho £13.2m
2. Carlo Ancelotti £11.4m
3. Pep Guardiola £11.2m
4. Arsene Wenger £8.3m
5. Louis van Gaal £7.3m
6. Fabio Capello £6.6m
7. Andre Villas-Boas £6.2m
8. Sven-Goran Eriksson £5.9m
9. Jurgen Klopp £5.3m
10. David Moyes and Laurent Blanc £5.1m
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment