RatibaKipindi cha Maswali ya Kawaida.
•Taarifa za Kamati za Bunge za Kisekta/ zisizo za Kisekta.
(i) Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala;
(ii) Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa;
(iii) Kamati ya Masuala ya UKIMWI.
Note:
TBC 1 Haitaonesha Bunge Badala yake itaonesha ziara ya raisi ya Ujerumani.
Spika anaingia saa 9:00 Asubuhi
Makamo wa mwenyekiti mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh Jafo anamuwakilisha mwenye kiti wa kamati hiyo Mh Lowassa.
Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi na Biashara
Maswali Ofisi ya waziri mkuu
Swali- Hilda Ngoye: Swali no(66).
JIbu- Aggrey Mwanri Naibu Waziri Mkuu: Swala la usafi wa miji linasimamiwa na sheria mbalimbali, serikali Inasimamia sheria hizi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.
Halmashauri zimekuwa na utaratibu wa kununua vifaa vya kufanyia usafi, Almashauri inatoza faini kati ya Tsh 10000 hadi sh 50,000 kwa mtu yoyote anayesababisha uchafu.
Ofisi inafanya ufatiliaji na kuwachukulia hatua watendaji wanaoshindwa kusimamia usafi.
Swali la nyongeza: Serikali imekuwa ikiratibu shughuri za usafi, je waziri anaweza kutuambia kuwa ameweka watu maalumu kwenye ofisi yake anayehusika na ufatiliaji wa shughuri za usafi ?
Waziri anaweza kuiangalia almashauri ya jiji la mbeya ili kuboresha zaidi ?
Majibu: Utaratibu uliopo kuna mtu anaitwa director of local goverment huyu ndio anahusika na shughuri hizo
Swali la nyongeza - Mh Mwanamrisho Abama: Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake linongozakwa uchafu je serikali inampango gani wa kuondoa tatizo hilo?
Jibu: Tunamradi wa Strategic cities, Tunamradi wa Dar ambao tumetenga zaidi ya Tsh Billion 5 kwaajili ya kuondoa tatizo hilo.
Swali la nyongeza - Mh Rajabu: Tunatatizo la kuwa na Dampo moja tu, kwanini Lisiwepo kwenye kila almashauri ?
Jibu: Majukumu ya kushughurikia taka yapo chini ya jiji, tutachukua haya mawazo yako na kuangalia uwezekano wa kuwa na madampo kila wilaya.
WIZARA YA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO
Anauliza kuhusu Waandishi wa habari kupigwa kwanini serikali isiwape ulinzi
Jibu- Naibu waziri Jumma Nkamia: Waandishi wa habari wazingatie sheria bila shuruti. Serikali katika matukio ya kitaifa huwa inawapatia waandishi mavazi maalumu ili kuwatofautisha na watu wengine.
Swali la nyongeza- Anna Malak: Waandishi wa habari huwa wanafata sheria na kuwa na vitambulisho lakini bado wananyanyaswa , wanapigwa na kupoteza maisha, lini serikali italeta bungeni mswada wa sheria wa kuboresha mazingira ya kazi.
Jibu- Naibu waziri Jumma Nkamia: Tatizo ni waandishi wa habari kukiuka sheria, na ni kweli waandishi wa habari some time wanakufa ila inabidi wachukue tahadhari.
:WIZARA YA NISHATI NA MADINI:
Swali- Kigola: Mheshimiwa raisi aliahidi kupeleka umeme kwenye vijiji vya malangali je serikali ni lini itapeleka vifaa kuanza kazi?
Jibu- Naibu waziri wa nishati na madini:
Swali la nyongeza: je vijiji vilivyo baki serikali itapeleka lini umeme ?
Jibu- Naibu waziri: Kunamaeneo hawajapeleka vifaa na kama ipo kwenye mpango wa kazi vifaa vitaenda. Transoma iliyoungua, Leo mje kuwauliza maswala ya transorma.
WIZARA YA AFYA USTAWI WA JAMII
Swali- Mh Sokoine: Serikali inawasaidiaje watoto wanalelewa kwenye makao ya watoto.
Jibu : Mh Kebwe: Kwa muujibu wa sheria ya watoto huduma zote za watoto zimewekwa chini ya wamiliki wa vituo, wizara inafanya ufatiliaji na ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha haki zote za watoto zinapatikana.
Swali la nyongeza- Mh Soni: Serikali inampango gani ili hawa watoto wanawekewa bima ya afya na inampango gani wa kusaidia vituoo visivyokuwa na mapato ya kutosha.
Majibu Naibu waziri: Serikali ipo kwenye utaratibu wa saidia vituo hivyo, na swala la bima ya afya ni mpango wa serikali kuwasaidia watoto hao.
Swali la nyongeza- Msabaa: Serikali inathamini kiasi gani mashirika ya dini na watu binafsi wanoajitolea kusaidia hawa watoto wasiojiweza?
Jibu- Naibu waziri: Nitaleta mchanganuo wa takwimu za kifedha za michango ya serikali.
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Swali- Abdalla Hajji : Baadhi ya wawekezaji sio waaminifu na wamekua wakiingia na siraha za moto nchini kinyume na sheria.
Jibu- Naibu waziri: Ni kinyume na sheria kuingia na siraha nchini, kwahiyo serikali inaomba mwananchi aliye na taarifa atoe kituo cha polisi.
Swali la nyongeza- Abdallaha Hajji: Lini serikali itakagua wawekezaji wote ili kubaini wawekezaji wanaomiliki siraha kinyume na sheria za nchi.
Jibu: Ni muhimu wananchi kushirikiana na jeshi la polisi wanapomtilia shaka mtu.
Swali- Mh Amina: Juzi kuna uhalifu wa kutumia siraha ulitokea Darajani je watuhumiwa ni watu wa Asili gani?
Jibu: Tar 23 Ni kweli lilitokea tukio la uahalifu pale Darajani na watu hao walikamata na asili yao ni Watanzania kabisa.
Swali: Mh anaweza kutupa takwimu za matukio ya uhalifu na jitihada za serikali za kukabiliana na uhalifu huo ?
WIZARA YA MAJI
Swali la nyongeza- Mh Mtinda: Almashauri ya wilaya ya Mkungi ni almashauri inayojitegemea kwanini bado almashauri hii haipewi ruhusa ya kuandaa miradi yake wakati ina vijiji 101, kawanini serikali isitoe ruhusa kwa almashauri hii iandae miradi yake ?
Majibu- Naibu Waziri Tamisemi: Sasa hivi kila almashauri inaandaa mipango yake, kwahiyo wanaruhusiwa kuandaa mipango yake.
Majibu ya swali la nyongeza: serikali bado inampango wa kujenga bwawa kwenye mto songwe na utathimini bado unaendelea.
Swali la nyongeza- Mh Kibona: Tangu mradi huu umeanza wananchi hawajashirikishwa kwa namna yoyote, je upotayari kuandaa utaratibu wa kuwaelimisha ili wajue ninini kinachoendelea kwenye eneo lao?
Majibu- Naibu waziri: Ni kweli wananchi wanapaswa kupata elimu ya mradi huu, na tupo tayari kuendelea na kuwaelimisha wananchi.
Swali la nyongeza- Mh Mogela: Juu ya tatizo la fedha zinazopangwa kwenda kwenye almashauri na fedha hizo hazifiki ?
Jibu: Fedha zimeshatoka.
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
Mh Mgondo Swali la nyongeza: Serikali imekuwa na tabia ya kuchukua maeneo ya wananchi kabla ya kulipa fidia. Kwanini wananchi wa king'ori na Malulla wasiruhusiwe kuendelea na shughuri za maendeleo?
Mh waziri Majibu: Wanaweza kuruhusiwa kutumia maeneo yale kupanda mazao ambayo sio ya muda mrefu.
Mh Liziwani swlai la yongeza: Pale bagamoyo kumekuwa na mpango wa EPZ, lakini ni muda mrefu sana hakuna kinachoendelea, nini mpango wa serikali juu ya eneo lile.
Jibu: Kazi inayoendelea muda huu ni kuangalia taratibu za kulipa fidia na tayari tsh billioni 6 kwaajili ya kulipa fidia.
WIZARA YA FEDHA
Swali- Mbunge wa Mbeya vijijini: Serikali inampango gani wa kuboresha viwango vya pensheni ?
Jibu- Naibu waziri wa fedha: Serikali inatambua umuhimu wa kuboresha viwango vya pensheni kwa wastaafu na ipo kwenye mpango wa kuboresha pensheni hizo.
WIZARA YA UJENZI
Swali- Mwaiposa Mbunge wa Ukonga: Serikali inampango gani wa kuruhusu kampuni za nje na za ndani kuwekeza kwenye mipango ya ujenzi wa barabara.
Jibu- Naibu waziri: Sheria ya PPP inaruhusu makampuni binafsi kushiriki katika miradi ya ujenzi wa barabara.
Jibu la swali la nyongeza: pamoja na mawazo mazuri uliyo nayo, bado tuliona mfumo wa PPP ni mfumo unaofaa zaidi.
Swali la nyongeza- Mh Mikidadi: Madaraja ya mkoa wa Lindi yalijengwa wakati wa mkoloni na kuendela , mengi ni mabovu, je serikali itafanya lini ukarabati?
Majibu: Ni kweli madaraja mengi ni ya zamani na yametumika kwa muda mrefu, kama nilivyosema kwenye swali la msingi , ni kazi ya TANROADS kufanya ukarabati wa madaraja haya.
KIPINDI CHA MASWALI KIMEISHA
Spika anatangaza wageni :
Katibu: Hoja Za Kamati
Mh Rwekiza Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Katiba, Sheria na Utawala anawasilisha ripoti ya Kamati
Michango ya wabunge (Kutoka ripoti za kamati 3 za Bunge za kudumu)
Mh Silinde: Lengo la TASAF ni kusaidia kaya maskini. TASAF inasema "Mpango huu unalenga kuzisaidia kaya 113" Bullion 31 zimegawiwa kwa kaya masikini. Mradi huu unatakiwa ufanyike sasa hivi ili fedha hizo zisitumike kama rushwa kwenye kipindi cha uchaguzi.
Taifa letu linashida la ajira, tunawasomi wanakosa vitu vya kufanya, wananchi wajue kuwa kunamgao wa fedha kutoka TASAF 3. Kupitia hiyo TASAF watu wapewe mikopo iwasaidie.
Kuhusu Daftari la kudumu la kupigia kura: Sheria inataka daftari liboreshwe kila baada ya miaka 2 na nusu. lakini mpaka sasa serikali bado haijatekeleza jambo hili. Hii inaonesha kuwa serikali inahofu kwani haijaboresha daftari hilo kwa zaidi ya miaka miwili.
Serikali itupe ufafanuzi kwanini wakurugenzi walifukuzwa kwenye matatizo yaliyotkea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, tunataka serikali itupe majibu.
Mh Augustino Masele: Napenda kuishauri serikali iziangalie kwa makini maeneo mapya ya utawala yapo kwenye mazingira magumu. watumishi hawaoni mbele kuna nini, watumishi wanaona kama wameadhibiwa kupelekwa kwenye maeneo hayo. Mfano kwenye wilaya yangu ya MBOGWE mpaka sasa hakuna shughuri yoyote ya ujenzi inayoendelea.
Serikali iharakishe mpango wa kuajiri watendaji wa kata na kijiji, ili waweze kuwa watumishi wa serikali na waweze kuwajibika vizuri kwenye shughuri za maendeleo.
Sheria ndogo ndogo- zinapokuwa zimepitishwa kwenye almashauri, upitishwaji wake kwenye ofisi ya waziri mkuu unachelewa sana.
Mapato na matumizi kwenye vijiji- Tunatatizo kubwa la matumizi ya fedha za serikali na zile zinazochangishwa na wnakijiji wenyewe, wananchi wanakata tamaa kutokana na matumizi mabovu ya pesa wanazochangia.
Katiba na sheria- Kuwepo kwa watendaji wazuri na wenye weledi ni jambo lisiloepukika, mahakama ziwezeshwe ziwe na majengo yanayoeleweka ili kuboresha huduma wanazotoa.
Nashauri tamisemi wawe na mipango ya kuhakikisha maeneo ya wananchi yanapimwa.
Mh Gaudence Kayombo: Nitajikita zaidi kwenye kamati ya TAMISEMI na hoja zote nazinga mkono. Kamati ya TAMISEMI kwenye ukurasa wa 13 kwenye ripoti yake, inaonesha kuwa fedha zinachelewa kufika, mimi naomba serikali iharakishe kufikisha fedha hizo.
Pili ni miradi kuchelewa kukamilika pamoja na matumizi mabaya ya fedha, mimi nashauri serikali iendelee kutoa adhabu za mara kwa mara ili kurekebisha matatizo haya.
Juu ya maeneo mapya, tunashukuru kwa kata mbili ambazo Mbinga tumezipata. Bado kuna maeneo yanastahili kupandishwa hadhin na kuwa vijiji.
Nikumbushe kuwa Mbinga kunanyumba ya muda mrefu ya DC inahitaji kama millioni 50 tu kuikamilisha ujenzi wa nyumba hiyo.
Mh Mipata: Wananchi wa Chala wanakero kubwa, wanasubiri fidia barabara yote wananchi wamepewa fidia lakini Chala bado hawajapewa fidia. Swala la mawasiliano ya simu. ninakata tatu kata ya kala mwampembe na ndimbo lakini mawasiliano hakuna.
Mradi wa king'ombe umeshakula zaidi ya millioni 500 lakini mpaka leo maji hakuna, hii ni aibu, tutawaambiaje wananchi ? watatuuliza tutashindwa kujibu. Mwisho ni swala la kilimo mwaka huu hamkutupatia mbolea kwaajili ya kilimo.
Sasa hivi wakulima hawatupigii kura, kwasababu mbolea mliyowawezesha kuwapa hamuwapi, mazao mnawakopa mmuwalipi kwa wakati, watoto wao wanaumwa hawapati matibabu watoto wao wanakufa, hawawezi kuwapa kura.
Spika: Wenye viti wa kamati na manaibu wao wanatakiwa kwenye kikao cha kamati ya uongozi.
SPIKA ANAGHAIRISHA SHUGHURI ZA BUNGE MPAKA SAA 11
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment