Sauti: Sikiliza Hoja Ya Mbunge Halima Mdee Iliyoibua Utata Mkubwa Juu ya ishu ya UDA na Chenge Kuhusishwa na Mikataba Mibovu

Kikao cha Bunge kilianza siku ya Jumanne January 27, Kamati mbalimbali zilikuwa zikiwasilisha taarifa za Ripoti tangu kuanza kwa kikao hicho, Kamati ya PAC iliwasilisha taarifa iliyotokana na Ripoti ya CAG ambayo ilibaini ubadhirifu kwenye taasisi mbalimbali, Wabunge wakaanza kuchangia kuhusu taarifa ya ripoti hiyo.

“Tulijadili ESCROW suala lilikuwa MAHAKAMANI, tulijadili LIPUMBA suala lilikuwa MAHAKAMANI leo tunakuja kujadili UDA ambalo lina mustakabali wa mkubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam mnasema suala liko MAHAKAMANI. Hili suala linazuiwa kwa sababu kuna wakubwa nyuma…”— Halima Mdee.

Mwenyekiti wa Bunge Mussa Zungu akamkatisha Mbunge huyo;“Mheshimiwa Halima we still respect you.. najua concern yako.. mimi sina tofauti na Jaji hapa, nikitoa ruling una sehemu ya kwenda kulalamika. Hili ni BUNGE la heshima na katika watu wanaheshimika wewe ni mmojawapo. Hoja za MAHAKAMA ziache!”

Halima Mdee aliendelea kuzungumzia ishu hiyo tena, Mwenyekiti huyo akamkatisha kwa mara nyingine; “Halima kama utakosa priviledge yako ntazuia… Hata mimi jana nimezuiwa, nimeanza ikabidi nisalimie watu nikakaa chini kwa kuheshimu mamlaka. Itabidi nifanye action ambayo sipendi kufanya, nna adi ya manjano na kadi nyekundu. Za manjano zishachoka sasa zinaanza kugeuka rangi.”

Baada ya hapo Halima Mdee akaendelea kuchangia; “ Ukiangalia nani ambaye alohusika kwenye mkataba wa 2007/08, Chenge alikuwa Waziri wa Miundombinu alikuwepo. Chengena mikataba ya nchi hii ya madini mibovu yupo.. na IPTL yupo… hatuchukui hatua mambo yanaenda tu. Mtafanya wananchi wataanza kuchapa watu barabarani, wakianza kuchapwa hawa nd’o discipline itakuja…”

Baada ya hapo Andrew Chenge naye alipata nafasi kujibu hoja ya Mdee; “Nimemvumilia sana mheshimiwa anayechangia hoja, kama ana ushahidi wa hayo anayoyasema kanuni zetu zinatutaka ayawasilishe tu mbele hapo”

“Kuna utaratibu wa kikanuni vielelezo nikitakiwa kuleta nitavileta haina tatizo”—Halima Mdee.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment