“Hakuna kitu kibaya kama siasa za kulipizana visasi, unaweza kukuta hata wale walioko madarakani hawana uhakika na wanaotaka kuja, kwamba hili litaendelea bila kulipizana visasi… Dhambi ya kulipiza visasi, majungu, fitna na uvivu wa kutofikiria, dhambi ya ubaguzi.. Tanzania yetu leo hii ni ipi?, hatuna itikadi, akiingia huyu ataendelea na pale mwenzake alipoishia”
Niombe watanzania kwa moyo wa unyeyekevu kutika ndani ya sakafu ya moyo wangu wachague viongozi wasiona mlolongo wa sifa nyingi, ziwe nne tu ya kwanza awe mwenye uwezo, pili mcha MUNGU, tatu awe mkweli.. aseme ukweli na si kutumia jukwaa la siasa kinyume, na nne mwenye kuchukia ufisadi…““Sakata la Escrow… maazimio haya yatekelezwe, la kwanza lilianza na wale wakubwa ingawa wote ni wachafu, huwezi kusema unashughulika na vidagaa na kuacha wale mapapa na manyangumi… Ujanja ujanja uliofanyika kodi haikulipwa, zile dola milioni 75 kodi yake iko wapi? Hatujaona mtu akikamatwa.. waliolisimamia hili walitakiwa wawe wameshakamatwa, huwezi kumkatama anayedaiwa dola 25,000… huko ni kukosekana uadilifu”
Kuhusiana na Kura ya maoni kwa Katiba iliyopendekezwa; “Kura ya maoni kwa mawazo yangu haiwezekani, leo hii hatuna daftari la wapiga kura na kama kuna tatizo litakaloikumba Tanzania na tukayumba kwelikweli tusipowekeza akili zetu zote tukawa na utulivu wa dhati zetu, ni daftari hilo…“
Daftari la mwaka jana NEC imesema daftari lile ni chafu… mfumo utakaotumika ni wa kielektroniki, kutumia mfumo wa kisasa, mfumo huo haujafanikiwa nchi za Afrika, Ghana, Msumbiji, Namibia, Afrika kusini”
Maoni yake kuhusu uandikishwaji wa daftari la wapigakura; “Tume ukiwauliza wamepewa fedha kiasi gani kwa sasa ni aibu kusema hadharani, wangeweza kutumia wanajeshi lakini kwanini uwaambie Watanzania wanataka kutumia wanajeshi? Wanaweza kuvaa nguo za kiraia na kufanya kazi hiyo? Hapa kuna walakini fulani, maandalizi ya kifedha ni shida, rasilimali watu kuiwezesha tume nayo ni shida, vifaa havijafika kwa sababu Serikali haijalipia fedha hizo ili viletwe…“
Faida ya kwetu kujiondoa kwenye mchakato huu ni faida kubwa zaidi kwa sababu tunnalipenda taiifa la Tanzania liwe la amani na utulivu…“– James Mbatia.
Credit: Milard
0 comments:
Post a Comment