Spika amemtangaza Sitta kukaimu uongozi shughuli bungeni kwani muhusika yuko safari.
Chibulunje: Ibara ya CCM inaitaka kutambua mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi, kitu gani kinashindikana.
Jibu: Kunahitajika maoni na maamuzu ya baraza la mawaziri ili muswada uje bungeni, Serikali imeshatoa agizo la kusimamisha ujenzi wa majengo mapya Dar es Salaam.
Chibulunje: Mchakato serikali ulioeleza si sababu za msingi kuchelewesha mchakato kwa miaka mitano, Je! Serikali haioni umuhimu wa kuharakisha mchakato kabla ya uchaguzi2015? Wizara bado zinajenga Dar es Salaam.
Jibu: Bunge kuwa Dodoma ni matokeo ya mchakato na azma ya serikali. Manispaa ya Dodoma tayari ina watu laki tano, tukihamisha zidisha mara kumi, sisi tunaenda kwa hatua kwa kuweka miondombinu ambayo itabeba watu watakaohamia. Kuhusu ujenzi DSM, naomba ushahidi na majengo hayo, isije ikawa mtu anajenga kareserch unit ukasema anajenga wizara.
Badueli: Kwanini serikali isiandae ratiba maalumu ya kuhama kwa hatua iletwe bungeni
Jibu: Ni jambo zuri na ushauri tumeupokea
Akunay: Kwa kuwa tayari imeshachukua miaka 43 na bado hatujafanikiwa, serikali haoni ni muda sasa wa kureview
Jibu: Siwezi kusema hapa kwa niaba ya serikali eti tumebadilisha, kama kuna haja tutakaa hapa. Kulikua kuna sababu ya kuhamisha makao makuu Dodoma, watu watatushangaa tukibadili msimamo wetu.
Faida Bakari: Je! Wafanyabiashara walemvu wangapi waliopata mabilioni ya Kikwete
Jibu: Mpango wa kuwawezesha wananchi kiuchumi ulikuwa na mpango wa kuongeza ajira bila kujali maumbile yao, Namshukuru Mh Mbunge kwa swali zuri na tumepokea kama changamoto.
Bakari: Kwa kua waziri amikiri mkopo hauna vigezo maalumu, imesababisha watu wengi wenye ulemavu kukosa. Nashukuru kuletwa vigezo, Je! Vitaanza lini?
Jibu: Kwanza hakuna vigezo kabisa, vigezo vilikuwa kwa mabenki. Tutarejea tena vigezo vile ili viwe rahisi kwa walengwa.
Msabaha: Mikopo ya JK na kwa ZNZ Karume, kuna watu hawakurejesha, serikali ilichukua hatua gani!
Jibu: ZNZ walipata milioni 600 na wenyewe waliongeza milioni 600. Mkaguzi wa ndani ameshafanya kazi kubaini nani amerejesha na wasiorejesha ili hatua zichukuliwa
Kulikoyela: Pensheni ni haki, serikali ina mpango wa kuwapatia pensheni wahadhiri wa vyuo waliokuwa kwenye mpango wa SSS waliostaafu kabla ya march 2011, pia wazee wote waliofikia umri wa kustaafu!
Jibu: Wahadhiri bado linashughulikiwa, serikali bado iko katika utafiti na majadiliano ili kulipa pensheni kwa wazee wote.
Kulikoyela: Maswali hayajajibiwa, swala la wahadhiri lipo sasa zaidi ya miaka 20, timeline ikoje? Tuliahidiwa na waziri mkuu mchakato wa kulipa wazee wote utaisha karibuni
Jibu: Mpango wa wahadhiri, katika kikao cha maraza la mawaziri, iliamuliwa kuwa wale waliokuwa wanafundisha mpaka 2011, wahamishiwe PPF na wataendelea kulipwa. Wa kabla walikataa PPF hivyo baraza la mawaziri lilikataa. Kuhusu la pili kuhusu wazee wote bado tunaendelea na utafiti. Vyanzo vya fedha havitoshi. Bado tunaangalia vyanzo vingine.
Swali; Kuna wafanyakazi zaidi ya 300 walioachishwa kazi kwenye mgodi wa Buliyngule baada ya kupata matatizo kazini, wanazungushwa sana, serikali inatoa kauli gani?
Jibu: Linashughulikiwa na wenzetu wa OSHA, ni swala lefu na siwezi kulingumzia hapa.
Swali: Mahakama zinatumia kiingereza, Je! Serikali haioni ni muda sasa kutumia Kiswahili
Jibu: Serikali inafahamu umuhimu, lugha za mahakama za mwanzo zitakuwa Kiswahili. Lugha inayotumika mahakama kuu ni Kiingereza ama Kiswahili ila kumbukumbu zitaandikwa kwa lugha ya Kiingereza.
Swali: Kutokana na usumbufu unaopatikana, serikali haioni ni muda sasa kulileta bungeni libadishwe
Jibu: Ni kweli kuna haja ya hukumu pia kuandikwa kwa Kiswahili, changamoto kubwa ni sheria zetu zipo kwenye lugha ya kiingereza. Tumeshaongea na TUKI pia baraza la Kiswahili. Pia miswada yote tunayoleta ina lugha Kiswahili pia.
Swali: Karagwe kuna adha kubwa ya maji, na mheshimiwa rais alipokuja alituahidi, lini ahadi itatekelezwa
Jibu: Ni kweli kuhusu ahadi, stadi imeshafanyika, utekelezaji tu unasuburiwa pindi fedha zitakapopatikana.
Swali: Kwanini inatokea kampuni zinasema gharama zake za simu ziko chini sana wakati TCRA inasema ni sawa!
Jibu: TCRA haipangi gharama za simu bali inapanga gharama za maunganisho kati ya mtandao mmoja na mwingine ambazo kwa sasa ni Tshs 30.58 kwa DK, gharama za ndani za mtandao mmoja zinapanga na mtandao husika hivyo ni wazi zitatofautiana, ikiwa mtandao unatoza zaidi ya bei elekezi ya TCRA hatua stahiki zitachukuliwa.
Silinde: Kwa kuwa kuna kitengo cha hujuma, kuanzia 2010-2013 kumekua na vocha bandia, kampuni ya Vodacom imeisimamisha shivacom kutengeneza vocha kwa kasha ya kutengeneza vocha feki zenye thamani ya $ nilioni 350. M-Pesa pekee zimepita trilioni 10, kwanini serikali isilete taarifa bungeni kujua mwenendo mzima wa fedha hizi?
Jibu: Swala la vocha bandia hatulijasikia, Mgogoro wa Shivacom na vodacom ni mgogoro wa kibiashara na hatujapokea malalamiko ya vocha feki. Kwenye mtambo mpya, kwenye hatua ijao tumeweka kifaa kuweza kubaini miamala iliyopita kupitia mitandao ya simu, hivyo serikali itajua kodi inayopaswa kulipwa.
Kitandula: Wizara ilinijibu kufikia Dec 31 itakua imeweka mnara wa simu kata ya Mwakijembe, kwa sababu za kiusalama, serikali haioni eneo hili linatakiwa kuwa na mawasiliano ya simu?
Jibu: Ni kweli tulimpa barua kumueleza kampuni ya Vodacom ni lini itaweka mnara, tuliandika kulingana na barua tuliopewa na Vodacom. Kulingana na matatizo kwenye makampuni yaliyopewa kazi ya kujenga minara, ilishindikana na tumeshaziagiza kampuni za simu zitafute wajengaji wengine.
Ayoub: TZ imekuwa na ushirikiano na uingereza kwa muda mrefu, kwanini ubalozi wa Uingereza umefungwa muda mrefu na kuleta adha!
Jibu: Ubalozi haujafungwa na wala hatutarajii, ni kweli huduma za viza zimeamishiwa kwa wakala, kutokana na maelezo ya ubalozi, pamoja na kuwa viza zinashughulikiwa, muda wa wastani ni siku 18 kabla ya safari. Tatizo litakuja endapo kuna safari ya Ghafla. Serikali inaendelea kufanya jitihada kupunguza adha ya kupata viza.
Nyongeza: Kwakua amekiri kuna uhusiano mzuri na Uingereza, huduma kufanywa na mawakala badala ya ofisi yenyewe huoni inajenga sura mbaya kwa watanzania. Swala la visa Nairobi, ni lini watakaa kikwelikweli kulitatua!
Jibu: Ni kweli huduma za visa zinatolewa na balozi husika, serikali ya Uingereza inajaribu kubana matumizi pia inaweka pamoja ili kudhibiti wageni wanaoingia uingereza ikiwemo Ugaidi na sasa wanashughulikia kwa pamoja Pretoria
0 comments:
Post a Comment