Chelsea Kuteta Faragha Na Fiorentina

Vinara wa ligi kuu ya soka nchini England, Chelsea wanajiandaa kufanya mazungumzo rasmi ya kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Colombia na klabu ya Fiorentina ya nchini Italia, Juan Cuadrado.
Chelsea wanajiapanga kukamilisha dili ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, baada ya uongozi wa klabu ya Fiorentina kuikubali ofa ya paund million 23 iliyowasilishwa mezani na The Blues.
Kabla ya kukubaliwa kwa ofa ya paund million 23, uongozi wa klabu ya Fiorentina ulikua unasisitiza ada ya paund million 26.8 ambayo ingetumika kwa ajili ya usajili wa Cuadrado.
Kwa juma moja sasa Chelsea walikuwa wanahusishwa na mipango ya usajili wa Cuadrado, huku ikielezwa kwamba kiungo André Schürrle kutoka nchini Ujerumani atalazimika kuuzwa kupisha ujio wa kiungo huyo ambaye alitamba wakati wa fainali za kombe la dunia.
Kama itakumbukwa vyema Man Utd walionyesha nia ya kutaka kumsajili Juan Cuadrado, wakati wa usajili wa majira ya kiangazi, lakini uongozi wa klabu ya Fiorentina ulikua imara kwa kukataa mpango huo usifanikiwe kwa kigezo cha kuhitaji kumtumia kwa msimu huu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment