Afya ya Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba imeelezwa kuimarika na kisha kufikishwa mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa shitaka linalomkabili.
Lipumba ambaye alikuwa akiohojiwa katika kituo cha polisi kati na kisha alipatwa ghafla na ugonjwa wa presha ya kushuka na kisha kupelekwa katika hospital ya UN Clinic kwa matibabu zaidi.
Mara baada ya kuimarika kwa afya yake amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kusomewa shitaka linalomkabili.
Akisoma shitaka wakili wa serikali Joseph Maugo mbele ya hakimu Mfawidhi Isaya Arufani, Prof Lipumba anadaiwa kuwashawishi wafuasi wa chama chake kufanya jinai kwa siku mbili tofauti yaani tarehe 22 na 27 mwezi huu.
Hata hivyo Mshitakiwa alikana mashitaka na yuko nje kwa dhamana ya wadhamini wawili kwa hati ya shilingi milioni 2 na kesi yake itasomwa tena Februari 26 mwaka huu.
Prof Lipumba anatetewa na jopo la mawakili wa Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA wakiongozwa na Mohamed Tibanyendela
Akiongea nje ya viwanja vya mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu Prof Lipumba aliwashukuru watu mbalimbali ambao wamekuwa nae bega kwa bega tangu jana na mpaka kumwekea dhamana.
Aidha alizungumzia afya yake na kuwataka Wananchi na wanachama wa chama chake papote pale walipo kuondoa hofu kwa kuwa hali yake inaendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment