Video: Ni Zamu Ya Spurs Na Sheffield United, Adebayor Out

Michuano ya kombe la ligi huko nchini England inaendelea tena hii elo kwa mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali kuchezwa jijini London ambapo Tottenham Hotspurs watapapatuana na Sheffield United katika uwanja wa White Hart Lane.
Meneja wa Spurs, Mauricio Roberto Pochettino Trossero amesema kikosi chake hakitokuwa na budi ya kuwaheshimu wapinzani wao wa hii leo, kutokana na kuamini kwamba kimefika katika hatua ya nusu fainali baada ya kupambana vilivyo katika hatua zilizopita.
Amesema anajua tayari mashabiki wengi duniani kote wamenyesha kukiamini kikosi cha Spurs kwa kukipa nafasi ya kushinda kwa urahisi, lakini yeye kama mkuu wa benchi la ufundi huko kaskazini mwa jijini London anajua ugumu wa soka na morari ya wachezaji wa Sheffield United.
Wakati huo huo Pochettino amekanusha taarifa za kuonyesha dharau dhidi ya mshambuliaji kutoka nyumbani Afrika katika nchi ya Togo Emmanuel Sheyi Adebayor kwa kumuweka benchi kwa kipindi kirefu.
Pochettino amesema taarifa za kudharauriwa kwa Adebayor klabuni hapo hazina ukweli wowote na anaamini mshambuliaji huyo bado ana uwezo mkubwa wa kucheza soka na kuisaidia Spurs.
Amesema mwishoni mwa juma hili amepanga kumtumia katika mchezo wa kombe la chama cha soka nchini England FA dhidi ya Leicester City.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment