Vurugu Zaibuka Upya Donetsk

Kwa uchache watu 13 waliuawa katika shambulio dhidi ya gari katika mji wa Donetsk, Alhamisi Januari 22 mwaka 2015.
Watu thelathini na wanne wameuawa ndani ya masaa 24 Mashariki mwa Ukraine. Hata hivyo wito wa kusitisha mapigano uliyotolewa Jumatano Januari 21 mjini Berlin na Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani, Urusi, na Ukraine umepuuzwa.
Shambulio baya lililosababisha maafa makubwa limetokea Alhamisi Januari 22 asubuhi katika mji wa Donetsk, Mashariki mwa Ukraine. Shambulio hilo limegharimu maisha ya watu 13, baada ya gari waliokuwemo kushambulio kwa bomu.
Shambulio limetokea katika kata ya Kusini Magharibi mwa Donetsk, kata ambayo ilikua bado haijaguswa na mapigano. Gari waliyokuwemo watu hao limeteketea.
Waangalizi wa jumuiya inayohusika na usalama na ushirikiano barani Ulaya wamefika eneo la tukio ili kujaribu kujua sababu za shambulio hilo.
Jeshi la Ukraine na waasi mara mara, wamekua wakitupiana lawama na kunyoosheana kidole kuhusika na shambulio hilo.
Ikijaribu kujitetea, Wizara ya ulinzi ya Ukraine imethibitisha kwamba eneo kulikotokea shambulio ni kwenye umbali wa kilomita 15 na eneo kunakopatikana askari wa Ukraine.
Jeshi limepata pigo kubwa kwa mashambulizi hayo yanaoendelea Mashariki mwa Ukraine. Wanajeshi kumi wa Ukraine waliuawa saa 24 zilizopita, huku askari wakiondoka katika uwanja wa Donetsk, na kwa sasa uwanja huo unadhibitiwa na waasi.
Waziri mkuu wa Ukraine ameishtumu Urusi kuhusika katika shambulio dhidi ya gari hilo liliyotokea leo Alhamisi na kusababisha vifo vya watu 13. Kwa upande wake, Urusi umelinyooshea jeshi la Ukraine kuhusika na shambulio hilo.
Credit: RFI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment