Sakata La Escrow: Kamishna Wa Kodi TRA Apata Dhamana

Meneja Misahama ya Kodi TRA, Kyabukoba Mutabingwa anayekabiliwa na kesi ya kupokea rushwa ya Sh bilioni 2 ikiwa ni sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow amepata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Aidha,  Bw. Mutabingwa alifanikiwa kuwa na wadhamini watatu wa kuaminika, waliosaini hati ya dhamana ya Sh milioni 340, alitoa hati tano za mali zisizohamishika zenye thamani ya Sh bilioni moja lakini hataruhusiwa kusafiri nje ya mkoa bila kibali cha Mahakama.

Katika mashitaka yake anadaiwa Januari 27,2014 katika Benki ya Mkombozi wilaya ya Ilala , alipokea Sh 1.6 bilioni kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya VIP ambaye alikuwa Mkurugenzi wa IPTL James Rugemalira.

Anatuhumiwa kupokea fedha hizo kupitia akaunti namba 00110202613801 ambazo ni sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kama tuzo kwa kuiwakilisha kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits ambayo ni mali ya Rugemalira mahakamani, kitu ambacho ni kinyume cha sheria.

Katika mashitaka mengine anadaiwa Julai 15,2015, Kyabukoba akiwa katika benki hiyo alipokea rushwa ya Sh milioni 161.7 , Agosti 26,2014 alipokea tena rushwa ya Sh milioni 161.7 na Novemba 14,2014 alijipatia rushwa Sh milioni 161.7 kupitia kwenye akaunti hiyo, kama tuzo kwa kuiwakilisha kampuni hiyo ya Rugemalira mahakamani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment