Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zambia, Honour Janza, ametaja sababu ya ubinfsi wa wachezaji wake ulikua chanzo cha kushindwa kutamba katika mchezo wa mzunguuko wa pili wa kundi la pili, katika fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Tunisia ambao walimaliza dakika 90 wakiwa mbele kwa mabao mawili kwa moja.
Chipolopolo walionekana kupata nafasi nyingi za wazi katika mchezo huo ambao walidhaniwa wangeondoka uwanjani kwa furaha, lakini mambo yalikua tofauti baada ya kushindwa kufikia lengo la kutumbukiza mpira katika nyavu za Tunisia baada ya kuongoza kwa bao moja kwa kipindi kirefu.
Janza, alisema wachezaji wake walionekana kuwa na uchu wa kutaka kufunga kila walipofika langoni mwa wapinzani wao, lakini walikosa umakini kwa kutanguliza maslahi binafsi.
Katika mchezo huo dhidi ya Tunisia, Zambia walitangulia kupata bao lililofungwa na mshambuliaji wa klabu ya Southampton ya nchini England Emmanuel Mayuka katika dakika ya 59, lakini Eagles of Carthage walisawazisha katika dakika ya 70 kupitia kwa Ahmed Akaichi kisha Yasine Chikhaoui akaongeza bao la pili katika dakika ya 88.
Wakati Zambia wakipoteza mchezo wao dhidi ya Tunisia, timu ya taifa ya Jamuhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo imeshindwa kutambiana na timu ya taifa ya Carpe Verde.
Kwa mantiki hiyo sasa Tunisia wanaongoza kundi la pili kwa kufikisha point nne, wakifuatia na Jamuhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo na Carpe Verde wenye point mbili kila mmoja na Zambia wanaburuza mkia wa kundi la pili kwa kumiliki point moja.
Hii leo michuano hiyo inaendelea tena kwa michezo ya kundi la tatu ambapo timu ya taifa ya Ghana itatupa karata yake ya pili kwa kupambana na vinara wa soka barani Afrika Algeria, mishale ya saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa de Mongomo, na kisha mchezo wa pili wa kundi hilo utashuhudia Afrika kusini wakipapatuana na Senegal katika uwanja huo huo uliopo mjini Mongomo.
0 comments:
Post a Comment