Siri Imevuja Kutoka Zanzibar Resort: Mwigulu Kung'olewa Kamati Kuu CCM, JK Ashinikizwa

KUVUJA KWA BARUA YA KINANA KWA MWIGULU NI NJAMA-VITA YA KUMSHINIKIZA JAKAYA KIKWETE AMNG'OE MWIGULU SEKRETARIET /KAMATI KUU.

Taarifa kutokaa ndani ya msafara wa katibu mkuu zinasema kuwa hii ni njia nzuri ya kumshinikiza mweneyekiti wa chama hicho Dr Jakaya Kikwete ya kumwondoa Mwigulu Kwenye Unaibu Katibu Mkuu. Mmoja wa maafisa wa juu wa chama hicho anayeambatana na Katibu Mkuu katika ziara za mikoani alinukuliwa akisema, tuna mshangaa sana Mwenyekiti, hata kama ni mapenzi kwa kijana wake yamezidi, maana tunasikia ni mwanae, tulikuwa hatumjui sijui kamtoa wapi, mara mchumi wa chama, mara Naibu katibu Mkuu, Mara Naibu Waziri, sasa ameshakuwa Serikalini kwanini hamwondoi? 

Maelezo ya ndg Mwigulu Nchemba kwenye vyombo vya Habari kuhusu Kutii kauli ya Katazo la kinana "hayo ni maelekezo ya kikazi kutoka bosi wangu, ni maagizo ya kiofisi, nitayatekeleza kama maagizo mengine, kikazi kuna wakati unatumwa kazi hiyo, kuna wakati unaambiwa uiache kazi hiyo", Siri imefichuka.

Kila kikao tunajua ndio cha kumwondoa anayeyusha. Ndio maana tumemlipua. Kila wakati anamsifia kijana wetu, kiboko ya upinzani mbona wengine walipopelekwa serikalini aliwaondoa kwenye chama? Sasa tuone ziara hatafanya sijui atamwacha akiwa anafanya kazi gani. Aliongea kiongozi huyo kwa sauti ya juu na ya hasira akiwa na wasaidizi wao katika hotel ya Zanzibar Rezort majuzi.

Tulimsikia mmoja wa wasaidizi wao alisema, katika vikao vitatu vya NEC vilivyopita, kulikwepo na vikao vizito vya kambi zinazotaka Mwigulu aondolewe kwenye nafasi yake, mkakaati ulitengenezwa wa kumshinikiza Mwenyekiti Dr KIKWETE amwondoe Mwigulu kwenye Sekretarieti. Ndicho alichosema kiongozi huyo kuwa mwenyekiti aliyeyusha na kuuzika mpango huo. Lakini sasa labda barua hii Mwenyekiti atashtuka ili amwondoe.

Uchunguzi unaonesha kuwa ukweli sio tu sababu ni Mwigulu kuonesha kwa kauli na mwendendo kuwa anautaka urais, kuna la ziada
Moja Mwigulu ameonekana kuwa na mvuto sana kwa vijana ndani na nje ya chama kutokana na misimamo yake ya kutetea wanyonge bila uoga. Na kwa nguvu ya hoja zake watanzania wengi na wabunge hufuata alichokisema, kambi zingine zimeona kuwa asipozuiwa kuzunguka hakuna mgombea atashindana naye. Kama ni kuutaka urais tu je Waziri mkuu naye atazuiwa kuzunguka? Makundi yaliyokuwa yakipanga kumshinikiza mwenyekiti kumtoa Mwigulu yalishapanga safu zote ili kujirahisishia namna ya kuingia kwenye uchaguzi.

Jitihada za kumtafuta Mwigulu Nchemba ili kusikia kauli yake zinaendelea. Kiukweli nadhani kinachotafutwa ni namna ya kumshinikiza Rais amwondoe kwenye nafasi tu kwani hata mimi siamini kama kweli watu hawa hawana kikao wala hawajapeana namba za simu, wala ofisi zao haziko jengo moja hata wasielekezane wao mpka barua hii isambae dunia nzima.

Credit: JamiiForum
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment