Zitto Achunguzwa Kuvuna PAP

Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC) ameanza kuchunguzwa na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa kwa kutuhuma za kutumia rafiki zake wakiwamo mawakili Beatus Malima na Albert Msondo , kupokea fedha kutoka Kampuni ya Pan Africa Power Solutions(T)Limited. 

Habari zilizolifikia Gazeri la Jamhuri zinaonesha kuwa April 3 na 8, 2014 kwa nyakati tofauti marafiki zake hao walipokea Sh. Milioni 10 na dola 5,000 kutoka Kampuni hiyo kwa niaba ya ZITTO.


Pia kupitia Kampuni yake ya Gombe Advisors and Leka Dutigite Ltd iliyosajiliwa BRELA kwa namba 92959 Agosti 13 , 2012 na kipindi cha miezi minne tu tangu iliposajiliwa ilianza kupata fedha kutoka Mashirika ya Umma tofauti na Kampuni za Watu wengine ambao hawana wadhifa kama alio nao.

Kampuni ya Leka Dutigite Ltd imepata zaidi ya sh. Mil. 12.2 kutoka Hifadhi ya Taifa ya Sadani na mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) , zaidi ya Sh. Milioni 80. Kitendo cha kupokea hizo na zile za IPTL ndivyo vinavyochunguzwa iwapo hakutumia nafasi ya PAC kwa manufaa binafsi.

Hapo chini ni baadhi ya nyaraka zinazofanya Mbunge wa Kigoma Kaskazini , Zitto Kabwe achunguzwe kutokana na madai ya kuchukua fedha Kampuni ya PAP

Chanzo: Gazeti la Jamhuri
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment