Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akila kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia katika sherehe za zilizofanyika jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish
Rais Lungu 58, aling’arisha sherehe hizo baada ya kuvaa suti rasmi (Presidential suit) rangi ya bluu, shati jeupe na tai nyekundu zilizobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi. Lungu aliambatana na mke wake, Eshter Lungu walipokuwa wanaingia viwanjani hapo huku wakisindikizwa na ulinzi mkali.
Akizungumza baada ya hafla hiyo, Sheria Ngowi alisema amefurahi kupata nafasi ya kipekee ya kumvalisha Rais Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake na kusema ni hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu wa mavazi wa kimataifa.
0 comments:
Post a Comment