Breaking News: Mh. Mbatia Azua Jipya Bungeni Kupelekea Bunge Kuhairishwa

Baada ya Mbatia kuleta hoja ya dharura juu nguvu iliyotumiwa na polisi kwenye maandamano ya CUF jana tarehe 27 January ili ijadiliwe na wabunge kama hoja ya dharura, spika Makinda aliamuru serikali ilete majibu kesho ndio ijadiliwe. 

Wabunge walisimama kushinikiza hoja ijadiliwe lakini Makinda aliendelea na msimamo wake wa hoja kujadiliwa kesho baada ya Serikali kuleta majibu, hapo ndipo sintofahamu ilipozidi na kuleta kutoelewana kati ya wabunge wa Upinzani na Spika. 

Ilibidi spika Anna Makinda kuahirisha bunge mpaka kesho lakini baadae akabadili na kusema saa kumi jioni leo hii.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment