Watu zaidi ya 40 waliokuwa safarini kutoka Tegeta kwenda ubungo wamenusurika kupoteza maisha baada ya basi waliokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na lori lililoonekana kuwa ni la jeshi na mmoja wa abiria kukatika baadhi ya viungo vyake vya mwili kufuatia ajali hiyo.
Ajali hiyo iliyotokea Tegeta ilizua taharuki kwa wapita njia na abiria waliokuwamo ndani ya basi hilo aina ya Kosta huku wengine wakipatwa na kiwewe cha kutaka kuruka kunusuru maisha yao huku ikisababisha majeruhi wa ajali hiyo na umati wawatu ukiwa umezunguka kuona kile kilichotokea.
Wakazi wa tegeta na maeneo jirani waliguswa kwa hisia tofauti baada ya kufika hapo katika eneo ilipotokea ajali ambapo walianza kutoa msaada kwa lengo la kuwanusuru manusura kupoteza maisha,baada ya Kosta hiyo kuonekana ikiwa imepondeka pondeka huku abiria waliokuwa wamekaa mbele karibu na Dereva kuonekana kuumia zaidi ambapo kijana mmoja aliyekuwa mbele alishindwa kutoka baada ya ajali nahivyo kufanyika jitihada za kumnasua.
Msaada wa kunasua majeruhi wa ajali hiyo waliokuwa wamebanwa ilifanywa na wasamaria wema Mafundi Gereji wa Tegeta huku wakitumia kifaa maalumu cha kukata mabati ya magari kukata bati la Kosta hiyo na hivyo kuweza kunusuru maisha ya abiria hao ingawa wengine kuionekana kuwa tayari baadhi ya viungo vya miili yao kuumia kutokana na kubanwa kwa muda na bati la Kosta hiyo kwa muda mrefu.
Sbm Broadcast Iliweza kumtafuta kamanda wa polisi wilaya ya kinondoni Kamilius Wambura kuzungumzia ajali hiyo ambapo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema taarifa zaidi juu ya ajali hiyo ataitoa baada kufanyika kwa uchunguzi wa kuweza kubaini kiini cha ajali.
Hata hivyo Baadhi ya Mashuda wa ajali hiyo wamesema kuwa kutokea kwa ajali hiyo kumetokana na Dreva walori hilo kushindwa kuweka tahadhari katika eneo hilo hadi kutokea ajali ambayo ingesababisha vifo vya zaidi ya mamia ya watu.
Aidha Madereva wa njia hiyo ya Tegeta wamepaza sauti zao kupitia ajali hiyo nakusema kuwa ipo haja ya serikali kuangalia namna ya kuweza kuweka njia ya Mzunguko maarufu kama(Round About)Lengo kubwa likiwa kunusuru ajali na pia kwa mabereva wanao kuwa wakigeuzia katika eneo hilo la Tegeta kwa Dharura,na hivyo kusema kufanya hivyo kuta saidia katika suala hilo la kutokea kwa ajali na hivyo kuwasisitiza askari wa usalama bara barani kuangalia endapo kutakuwa na magari Aina ya lori kama hilo waweze kuchukua tahadhari mapema kabla Haijatokea ajali inayogharimu maisha ya abiria wasio na Hatia.
Credit: tambarare halisi
0 comments:
Post a Comment