Dr Slaa Alaani Kupigwa, Kuteswa na Kukamatwa Professor Lipumba !!..

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amelaani vikali unyama aliofanyiwa Mwenyekiti wa CUF Professor Ibrahim Lipumba hapo jana.

Dr Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa UKAWA amesema wanachama wa CUF walikuwa na haki Kikatiba ya kuandamana kuwakumbuka watanzania waliouawa Zanzibar mwaka 2001.

Dr Slaa ameshtushwa na kitendo cha polisi kuwavamia kinyama na kuwapiga vibaya waandamanaji ambao hawakuwa na silaha yoyote.

Kiongozi huyo wa upinzani amemtaka Rais Kikwete kujifunza kutoka mataifa mengine jinsi yanavyoheshimu maandamano na demokrasia hasa kwa vile amekuwa akizunguka mataifa mbalimbali duniani.

Source:Mwananchi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment