Wafuasi 30 wa Prof Ibrahim Lipumba Wasomewa Mashataka

Wanachama 30 wa chama cha wananchi (CUF) pamoja na  naibu mkurugenzi wa oganaizesheni, uchaguzi na bunge Shaweji Mketo na mkurugenzi wa mawasiliano Abdul Kambaya jana walifikishwa kortini kwa tuhuma za mashtaka matatu likiwemo la kufanya mkusanyiko usio halali.
Kwa  mujibu wa wakili wa serikali Joseph Maugo alidai mbele ya hakimu Emilius Mchauro wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu, jijini Dar es Salaam kuwa washtakiwa wanatuhumiwa kwa mashtaka matatu ambapo shitaka la kwanza linawakabili washtakiwa wote ambao wanatuhumiwa kula njama ya kufanya uhalifu. Shitaka la pili linawakabili washitakiwa 28 ambao wanatuhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali.
Ilidaiwa kuwa walifanya mkusanyiko huo januari 27 mwaka huu, wakiwa katika ofisi ya CUF iliyopo karibu na hospitali ya Temeke bila uhalali wowote walifanya mkusanyiko wa nia ya kufanya maandamano kuelekea viwanja vya Zakhiem, Mbagala, Dar es Salaam.
Mchauro amelima ili washtakiwa waweze kutoka kwa dhamana wanatakiwa wasaini dhamana ya sh. 100,000 na mdhamini mmoja wa kuaminika, lakini washtakiwa walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande.
Washtakiwa hao watarudishwa mahakamani januari 30 ili kuangalia kama wametimiza masharti ya dhamana, baada ya barua za wadhamini kwenda kuhakikiwa na upande wa mashtaka.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment