Joel Campbell Hajui Mustakabali Wake Arsenal

Wakala wa mshambuliaji kutoka Costa Rica Joel Campbell, yupo safarini kuelekea nchini England, kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Arsenal ambayo yataamua mustakabali wa mchezaji huyo.
Pamekua na hali ya sintofahamu katika mustakabali wa Campbell tangu msimu wa usajili wa majira ya baridi ulipoanza mwanzoni mwa mwezi huu, ambapo vyombo vya habari vya nchini England vimekua vikiripoti taarifa tofauti zinazomuhusu mshambuliaji huyo.
Hata hivyo bado haijafahamika kama kuna ukweli wa taarifa za kuuzwa moja kwa moja ama kupelekwa kwa mkopo katika klabu itakayoonyesha nia ya dhati ya kufunga dili na uongozi wa klabu ya Arsenal dhidi ya Joel.
Hata hivyo taarifa nyingine zinaeleza kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, huenda akatumika katika mpango wa usajili wa beki kutoka nchini Brazil, Gabriel Paulista ambaye yu njiani kujiunga na Arsenal katika kipindi hiki.
Mbali na taarifa hiyo pia meneja wa klabu ya Real Sociedad, David Moyes amekua akihusishwa na mpango wa kutaka kumsajili Campbell kwa njia yoyote ile, lakini Arsenal wamekua wagumu kuonyesha kama wapo tayari kufanya biashara hiyo.
Campbell, alitarajiwa huenda angekua katika kikosi cha kwanza cha Arsenal msimu huu, baada ya kuonyesha kiwango kizuri wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014, lakini hali imekua tofauti kutokana na ushindani uliopo huko Emirates Stadium.
Tayari Lukas Podolski na Yaya Sanogo wameshatolea kwa mkopo kwa kununuliwa na klabu za Crystal Palace pamoja na Inter Milan, hali ambayo bado inaendelea kuonyesha kizungumkuti kwa Campbell kama ataweza kubaki kutokana na safu ya ushambuliaji kupungukiwa watu wawili.
Wengine waliobaki katika safu ya ushambuliaji klabuni hapo ni Olivier Giroud, Danny Welbeck pamoja na Alexis Sanchez, hivyo kuna wasi wasi kwa Campbell kubaki na kutumiwa kama mshambuliaji chaguo la nne.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment