Yanayojiri Bungeni Dodoma: Alhamisi, January 29, 2015

Leo Bunge linaendelea pia, Kama jana Spika alivyosema, Leo Bunge litaanza ratiba upya. Ratiba inaonesha hivi;

· Kipindi cha Maswali ya Kawaida (Leo Alhamis ni Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu)

· Taarifa za Kamati za Bunge zinazosimamia Fedha za Umma.

(i) Kamati ya Hesabu za Serikali;
(ii) Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa;
(iii)Kamati ya Bajeti.

Vilevile Kama Spika Anna Makinda alivotangaza jana, Leo tunategemea Serikali ilete Majibu kuhusiana na Hoja Binafsi aliyo itoa mbatia akilalamikia Polisi Kuwakamata na Kuwapiga Wafuasi wa CUF akiwemo Mwenyekiti wake Prof.Lipumba.
============================== ======

Maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu

Swali- Zungu: Kuhusu sera ya mkurabita ambayo imeigwa mpaka Kenya na Wenzetu wanakusanya mpaka Tsh trillion 8. Nchini kwetu bado wafanyabiashara wadogowadogo wananyanyaswa kila kukicha, Tunakuomba Mamlaka zako zikae na wadau ili wafanyabiashara hawa wafanye biashara kwa amani ndani ya nchi yao, Tunaomba kauli ya serikali


Jibu- Waziri mkuu : Katika mazingira yetu ni vizuri mamlaka za mikoa na wilaya zishirikishe wadau hawa, mimi naamini yote yanaweza kurekebishwa kwa kupanga pamoja na kuweka mipango mizuri. Huu utaratibu upo hata ulaya. Natoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kukaa na vijana na kupanga nao taratibu hizo. Kwa upande wa ilala tutakaa pamoja mimi na wewe mbunge wao na wadau wengine ili tuweke mipango ya pamoja.

Swali la nyongeza: Usafi wote tunaupenda lakini zoezi linaloendelea sasa hivi ni unyanyasaji wa wanyonge. Watu kuporwa mali, hawa vijana wanategemewa na majukumu, nakuomba waruhusiwe kufanya biashara zao mpaka saa kumi pale kariakoo.

Jibu: Nakubaliana na Wazo lako, na wale wote waliohusika kwenye unyanyasaji wachukuliwe hatua

Swali- Halfani Hilali: Kuhusu sera ya serikali ya kilimo kwanza, na kilimo bila ardhi hakipo , kumekuwa na mgogoro wa Ardhi wilaya ya Sumbawanga, malonje na serikali bado haijatatua mgogoro huu, nini kauli ya serikali kwenye mgogoro huu.

Jibu: Ni kweli mgogoro huu haujaisha ila serikali inafanya jitihada za kuimaliza mapema.

Swali- Ngonyani: Mwaka 2015 ni mwaka wa uchaguzi mkuu, Mji wa mombo uliomba kuwa almashauri na serikali ilikagua na kuona vigezo vyote vimekamilika.

Jibu: Naomba unipe muda nifatilie nitakupa jibu.

Swali- Mnyaa: Kuhusu NIDA Na Vifaa vya Biometric.

Majibu yametolewa na waziri Mkuu.

Wameuliza Maswali watu sita tuu;


MASWALI YA KAWAIDA- OFISI YA WAZIRI MKUU

Swali- Mbowe: Mh Spika, katika majibu ya waziri anashauri almashuri zitenge fedha za kutosha kwenye kuondoa taka wakati anajua hali ya kiuchumi kwenye almashauri zetu ni mbaya, kwanini serikali isiweke comitment ya kubadili taka hizo kuwa mali na kutumika kwa shughuri zingine?

Jibu: Kwenye sheiria ya mazingira ya mwaka 94 inaelekeza kila almashauri iingize maswala ya usafi kwenye mikakati yake ya maendeleo. Lakini shughuri za rescycling zinafanyika na zinaruhusiwa.


OFISI YA RAISI UTAWALA BORA

Swali la Mh Merriam Msaba:

Jibu: Serikali inayo mamlaka ya kupokea matamko ya watumishi wa umma, tathin iliyofanyika mwaka 2013 inaonesha zaidi ya 75% ya matamko yalikuwa sawa, na hivyo hakuna kiongozi aliyetoa matamko ya mali zake ambazo ni za uongo.

Swali la nyongeza: Kunaviongozi na wafanyabiashara wakubwa wamewekeza fedha zao hapa na watanzania wamenufaika. Moja kwanini viongozi wanaowekeza fedha zao nje ya nchi wasiwekeze ndani ili taifa linufaike?

Majibu- Naibu waziri: Zipo sheria za kuzuia na kupambana na rushwa inasema iwapo mtumishi wa uma anagundulika kupata mali zisizo za halali basi mali zake zinaweza kutaifishwa na pia anaweza kufunguliwa mashtaka na tayari kuna zaidi ya kesi tano mahakamani.


WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTOSwali moja.


WIZARA YA FEDHA

Swali La Kigwangala.

Jibu: Chanzo kikuu cha mapato ya serikali ni Kodi, ni kweli wananchi wanachangia malipo kwenye baadhi ya huduma zinazotolewa na serikali, kwa gharama ndogo sana ukilinganisha na mahali pengine. Serikali inatoa Elimu ya sekondary bure japokuwa kuna mchango kidogo unaotolewa na serikali.

Swali la nyongeza: Kwanini serikali iliyopewa mkataba na wananchi ya kutoza kodi na kusimamia maendeleo kwanini serikali iendelee kuchangisha wananchi tena kwa kutegemea michango ya wahisani wakati inakusanya kodi ?

Jibu- Naibu waziri: Bajeti yetu bado ni ndogo kwahiyo serikali yetu inahitaji vyanzo vingine vya mapato ili kukidhi huduma hizo. Bado serikali itaendelea kutegemea michango ya wahisani na ya wananchi ili kukidhi huduma.


WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Swali - Mh Shabiby: Kuhusu Mradi wa REA:

Jibu Naibu waziri nishati na madini: Serikali imeagiza miradi yote ya umeme ikamilike ifikapo mwezi juni mwaka huu.

Swali la nyongeza: Kwanza siridhiki na haya majibu, kwakuwa ninauhakika kuwa mkandarasi hajasaini mkataba kwenye haya maeneo, Je mpo tayari twende Gairo kuhakiki kama wamesaini?

Majibu: Tutaenda jumamosi kuhakiki kama kazi hiyo inaendelea, TANESCO ndio mnajukumu la kutekeleza miradi hii ya REA kwahiyo ihakikishe inashirikiana vizuri na wabunge wa maeneo husika.


WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment