Yaliyojiri Bungeni Dodoma Leo

Taarifa za Kamati za Bunge zinazosimamia Fedha za Umma.
(i) Kamati ya Hesabu za Serikali;
(ii) Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa;
(iii)Kamati ya Bajeti.
============================== ===

MASWALI NA MAJIBU


Msigwa:
 Hakuwepo hivyo swali kuulizwa kwa niaba ni kuhusu mfuko wa wanawake.

Jibu: Ni kweli mfuko wa wanawake ulianzishwa mwaka 1963, halmashauri nyingi hazitengi fedha za kutosha hivyo kusuasua ikiwemo halmashauri ya Iringa

Selasini: Hadi sasa kiwango cha fedha ambacho kimerejeshwa ni kiasi gani ili zikopeshwe.

Jibu: Serikali ina nia ya dhati kuwawezesha kina mama na vijana, Wizara wajibu wetu ni kusimamia ili pesa zitengwe. Tuna udhaifu mkubwa wa hizi pesa kurejeshwa ili wapewe wengine. Bado ukusanyaji na utendaji unaendelea.

Kakoso: Swali kuhusu wakulima wa tumbaku juu ya ushuru wanaotozwa

Jibu: Ushuru wa mazao unatozwa kulingana na sheria, ushuru ni kati ya asilima 3-5. Imeandaliwa sheria ndogo ambacho kiwango cha ushuru ni 5% ya kununulia mazao kwa ajili ya halmashauri. Kuna tafiti imefanyika jinsi ya kutoza vizuri tozo za halmasauri na itawasilishwa bungeni ila kwa sasa tutatumia zilizopo.

Kakoso: Atueleze ni lini ataleta sheria ya mabadiliko

Jibu: Baadaya ya kufanya utafiti tunaandaa utaratibu wa kuleta bungeni, tutakutana na wizara ya kilimu tupate jibu la pamoja.

Swali: Serikali wanaweka viwango vya juu kwa halmashauri ukusanyaji mapato.

Jibu: Viwango vinapangwa na halmashauri yenyewe, serikali wanavipitia kama vinaakisi uhalisia na tunasisitiza kutafuta viwango mbadala

Josephat Nyerere: Uwanja wa Musoma ni kati ya viwanja kumi vilivyotakiwa kutengenezwa, Kazi itaanza lini

Jibu: Kinatakiwa kukarabatiwa na kuwekewa lami, serikali inafanya jitihada na miongoni mwa viwanja 11 vinavyofanyiwa tathmini kwa ushirikiano na benki ya dunia, usanifu unaendelea na utamalizika June 2015.

Nyerere: Sina swali jingine kwa sababu ni ahadi ya muda mrefu isiyotekelezeka

Kibona:
 Lini serikali itakamilisha uwanja wa Mbeya hasa swala la Taa

Jibu: Uwanja wa Songwe haujakamilika kama tunavyohitaji kama jengo la uwanja wa ndege, zimamoto na taa pia zipo katika program ya matengenezo.

Swali: Kiwanja cha Musoma hakiridhishi, ni lini serikali watajenga uwanja serengeti ili watalii watumie badala ya viwenja vya karibu

Jibu: Program ya sasa ni kuhakikisha viwanja vyote vinatengenezwe ikiwemo cha mkoa wa Mara, Kiwanja kipya kinahitaji mkakati. Halmashauri ya wilaya ya serengeti walimpata mwekezaji wa kujenga lakini hawakupata ushauri wa kutosha hivyo pesa zilizotolewa na mwekezaji hazikutosha.


Mshama: Napenda kujua maeneo mengi Nkenge kuna watu wameweka nyaya kwenye nyumba zao lakini hawapati umeme

Jibu: Maeneo yote tuliyojipangia kufikisha umeme, tutafikisha kabla ya 30 June, kwa sehemu umeme ulipofika wapeleke maombi ya kuunganishiwa kwa meneja wa TANESCO.

Matiku: Kwanini serikali imeruhusu shughuli za uchimbaji Nyabigina unaofanywa na Barick

Jibu: Mgodi wa North Mara uliwalipa fidia wananchi wote ambako shule ya Nyamigena, kampuni imetenga milioni 600, kinachosubiriwa ni halmashauri wachague eneo linalofaa. Kuna wananchi hawatafidiwa kwa sababu waliotakiwa wameshafidiwa. Si kweli kwamba serikali serikali imeshindwa kusimamia ulipaji fidia ila kuna watu wanataka fidia kubwa.

Nyongeza: Majibu ya waziri hayaridhishi na kufedhehesha, majibu ya meneja wa mgodi ni tofauti na akasema shule haihamishwi bali inakarabitiwa. Wananchi wa Tarime mmewafanyia tathmini miaka miwili sasa na huwa wanakamatwa na polisi wa task force.

Jibu: Nimshangae kusema majibu yetu si sahihi, serikali inaongozwa na sheria. Ndio zinazoongoza wananchi wafidiwa namna gani, mmoja tu aliomba ajengewe nyumba. Tathmini iliyofanyika waliikataa.

Lissu: Fidia kwenye maeneo ya madini ni tatizo kubwa ikiwemo jimbo langu, 2006 watu wengi waliondolewa kwenye maeneo yao na hakuna hata mmoja hata mmoja alielipwa mwaka wa nane sasa. Je huu ndio utaratibu?

Jibu: Nafahamu ishu ya Shanta mining kwa sababu Tundu Lissu alielekeza wananchi wakavamie huo mgodi. Kampuni ya Shanta ikiwa tayari haitaanza bila kulipa fidia.


Muyogela: Serikali imwekeza pesa nyingi katika miradi lakini wananchi bado, nini mpango wa serikali!

Zambi(Jibu): Serikali imekuwa ikiwafundisha wakulima kwa lengo la kuongeza uzalishaji na tija, inaajiri maafisa ugani, serikali pia imeshirikia na JEICA na tija imeongezeka. Serikali imeendelea kuboresha chuo cha Mbondo kukiwezesha kutoa mafunzo kwa ufanisi na ili kupata wataalamu bora.

Nyongeza: Ili vijana waze kunufaika na chuo cha Mbondo, serikali haioni umuhimu wa kurejesha masomo mashuleni kama zamani ili wakimaliza waweze kujiajiri.

Jibu: Nakubaliana na yeye, wanafunzi wanasoma nadharia na vitendo.

Mtevu: Jiji la Dar es Salaam kuna matatizo ya malipo mfumo wa Epica

Jibu: Ni kweli kulikuwa na matatizo, kulisababishwa na kuhamishwa kwa mfumo wa mawasiliano ili kutumia mkongo wa taifa ili kuimarisha.

Mtevu: Tatizo limepungua kwa kiasi kikubwa, lakini hata hapa bungeni lipo hilo tatizo, hatujui tunalipwa lini.

Jibu: Tangu kuhamishwa matatizo yamepungua, maeneo mengine tuna baadhi ya watendaji kwa sababu zao wenyewe wanasingizia mfumo

Makinda: Swala la bunge lina utaratibu kwa sababu tunafanya mpango bunge liwe na mfumo wake ndio maana kuna matatizo hizi siku mbili.

Mwatuka: Vituo vingi vya polisi Mtwara havina nyumba za polisi hivyo kuishi uraiani, inaleta tatizo pale wenye nyumba wanapopelekwa polisi

Jibu: Ni kweli wengi wanaishi uraiani badala ya kambani, askari anatakiwa afanye kazi kwa weledi na hadi sasa hamna ushahidi kwa askari polisi kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya mahusiano yao kwenye makazi

Makinda: Utambulisho na matangazo

Mbatia: Kujadili jambo la dharura kama kanuni ya 47 inavyoniruhusu(Anazitaja kanuni husika).


(Makinda anamruhusu kuendelea) Mheshimwa spika jana tarehe 27 mwenyekiti wa chama cha CUF alikua na ratiba ya mkutano wa hadhara na maandamo pia walifata taratibu zote za kisheria, cha kushangaza jeshi la polisi dakika za mwisho waliamuru yasitishwe, Lipumba alionyesha ushirikiano wa kusitisha lakini baadae kidogo jeshi la polisi waliamua kutumia nguvu kwa wananchi waliokuwa wametulia ikiwemo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. 

Jambo hili linaondoa utulivu na amani iliyopo. Jeshi la polisi lenyewe jana lilisema wamepewa maagizo kutoka juu. Hili ni jambo ambalo halikubaliki. Prof Lipumba wa chama chenye wabunge wengi, chama chake kinashiriki umoja wa kitaifa Zanziba, kama yeye anaweza kufanyiwa hivyo tutegemee nini kwa wananchi wengine. 

Kwa kuwa wamesema ni agizo kutoka juu tunataka kujua hilo agizo kutoka juu limetoka kwa nani na kwa maslahi ya nani, tulijadili jambo hili kama ilivyo bunge ni cha kuisimamia na kuishauri serikali. Naomba kutoa hoja.

Makinda: Naomba mkae, hoja hii haiungwagi mkono na mimi sio Kangaroo court(Mahakama ambayo haitendi haki). Someni kanuni na sehemu inasema spika atakavyoona na kuzingatia mazingira yatakavyokuwa, kwa mazingira haya naiagiza serikali kesho itoe kauli kamili ambayo sisi tutaelewana alafu kesho mimi ntaruhusu mjadala. Kama mnataka kufanya mnavyotaka fanyeni lakini hamtumii busara, kama unataka kutoka unaweza kutoka. Anajitahidi kuendelea na ratiba lakini makelele yanazidi.

Wabunge wamesimama bungeni na wanagomea kikao kuendelea.

Ninachosema jambo hili ni kubwa sana hivyo ni vizuri wote wakaelewa na nikasema naitaka serikali kesho.

Baada ya sintofahamu ya muda, naahirisha bunge mpaka keshona kubadili hivyo kuahirisha mpaka saa kumi.

BUNGE LIMEAHIRISHWA MPAKA SAA KUMI JIONI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment