Gonola Akanusha Kujitoa Uraisi FIFA

Gwiji wa soka kutoka nchini Ufaransa, David Ginola amekanusha taarifa za kujiondoa kwenye kinyang’anyoro cha urais wa shirikisho la soka duniani FIFA kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari jana jioni.
Ginola amekanusha taarifa hizo na kusisitiza bado anaendelea kwenye mchakato wa kuwania kiti cha urais wa FIFA, ambacho kwa sasa kinakaliwa na Sepp Blatter kwa vipindi awamu tano mfululizo.
Ginola amesema ameshangazwa sana na taarifa zilizotolewa katika vyombo vya habari hapo jana, na hajui ziliztokea wapi huku akisisitiza huenda kuna kundi la watu linataka kumuharibia mipango yake katika mchakato wa uchaguzi wa FIFA.
Gwiji huyo mbae aliwika na klabu za Tottenham Hotspurs pamoja na Newcastle Utd zote za nchini England amekanusha uvumi huo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.
Gwiji mwingine wa soka aliyejitokeza siku mbili zilizopita katika mbio za kuwania urais wa FIFA ni aliyekua kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ureno LuĂ­s Filipe Madeira Caeiro Figo.
Figo anakuwa mgombea watano kujitokeza hadharani na kutangaza nia baada ya kutanguliwa na Ali Bin Al-Hussein kutoka Jordan, Jerome Champagne kutoka nchini Ufaransa, Michael van Praag ambaye ni rais wa chama cha soka nchini Uholanzi pamoja na Blatter mwenye umri wa miaka 78 aliesisitiza kutetea kiti chake kwa awamu nyingine.
Kamati ya uchaguzi ya FIFA inatarajia kukutana februari 8, kwa ajili ya kujadili majina wagombea na kujiridhisha kama wametimiza vigezo vya kuwania nafasi hiyo nyeti ndani ya FIFA
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment