Makinda: Siwatambui Chenge, Ngeleja

Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema hawatambui wenyeviti wa kamati tatu za kudumu za Bunge ambao Bunge liliazimia wavuliwe nyadhifa zao kutokana na kutajwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow. Pamoja na kuwapo kwa maagizo ya Bunge, baadhi yao wanaendelea kujinasibu kuwa bado ni wenyeviti huku mmoja wao akiongoza vikao vya kamati.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Makinda alisema anachofahamu ni kuwa wenyeviti hao tayari wamaeshajiuzulu na kamati zao zinatakiwa kufanya uchaguzi wa wenyeviti wengine. Wanaotakiwa kuachia nyadhifa zao ni Victor Mwabalaswa (Nishati na Madini), Andrew Chenge (Bajeti) na William Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala), ambaye hadi jana mchana alikuwa akiongoza kikao cha kamati hiyo.

Siku tano zilizopita Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah alieleza kuwa kamati hizo zinatakiwa kufanya uchaguzi na kwamba wenyeviti hao hawakutakiwa kuongoza vikao, lakini hadi jana, hakuna uchaguzi wowote uliokuwa umefanyika na baadhi wanaendelea na majukumu yao.

Katika mkutano wake wa 16 na 17, Bunge katika azimio lake la tatu, liliazimia kuwa watu walioshiriki katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow wakiwamo viongozi wa kamati hizo tatu, wachukuliwe hatua kabla ya kuanza kwa mkutano wa 18 wa Bunge unaotarajiwa kuanza Januari 27.

Ngeleja alikaririwa na gazeti hili hivi karibuni akisema kwamba anaendelea kushikilia nafasi hiyo kwa maelezo kuwa uchunguzi sakata hilo bado unaendelea na ikithibitika ndipo Bunge litachukua uamuzi ambao alisema atakuwa tayari kuutekeleza.

Chanzo: Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment