Mama Aua Wanaye Wawili na Kuwafukia Ndani

Katika hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili mmoja wa miaka minne, na mdogo wake wa miezi minne wameuawa na mama yao, Zuhura Steven,  aliyedhaniwa  kutokuwa na akili timamu,  na kufukiwa katika mashimo mawili tofauti.


Watoto hao wamefukiwa katika nyumba walimo kuwa wakiishi iliyoko katika mtaa wa Salmini kata ya Chemchemu Manispaa ya Tabora

Wakizungumzia tukio hilo linalodhaniwa kutokea kuanzia asubuhi ya terehe 25/01/2015, hadi walipogundua tukio hilo usiku wa saa moja, Mwenyekiti wa mtaa wa Barehani pamoja na wananchi walioshuhudia tukio hilo, alisema kuwa watoto hao hawakuonekana wakicheza kama mazoea yao,

Aidha Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora kamishna msaidizi Juma Bwire, pamoja na matukio kadhaa yaliyotokea, Jeshi la polisi linasikitishwa na tukio hilo  la kikatili, ambapo alisema upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Amewataja marehemu kwa majina kuwa ni Mwamvua Mrisho (miaka 4) na Soud, ( miezi 4).
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment