Chama cha ACT, Tanzania Yatoa Taarifa kwa Umma Juu ya Kudhalilishwa Lipumba


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI,

CHAMA cha Alliance For Change and Transparance( ACT- Tanzania.)kiki zingatia msingi wa utu na uzalendo kwa taifa,kime pokea kwa masikitiko tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof.Ibrahim Lipumba huko mtoni Mtongani Katika Wilaya ya Temeke. jijini Dar esSalaam jana.

Msingi wa kukamatwa Prof Lipumba na wenzake ni kwa ajili ya kuadhimisha kumbu kumbu ya mauaji ya Watanzania Wenzetu yaliyofanywa na jeshi la Polisi miaka 14 iliyopita wakati watanzania hao wasio na hatia walipotumia haki yao ya kidemokrasia kufikisha ujumbe kwa serikali kwa njia ya maandamano.

Kama iliyokuwa miaka 14 iliyopita kwa jeshi la Polisi kushindwa kutumia weledi wa kazi yao na kujiepusha na mihemko ya kisiasa jana tena wameendeleza uoneu wao kwa watanzania katika jitihada za kuminya Demokrasia na kufikisha mawazo huru kwa watawala wetu kwa kisingizio cha uwepo wa tishio la Ugaidi.

Kwa kutumia hoja dhaifu na visingizio vilivyo jaa mihemko ya kisiasa jeshi la Polisi likajiingiza katika kuwakamata na kuwadhalilisha viongozi wa (CUF), lengo likiwa ni kuwatisha watanzania hasa wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais Madiwani na wabunge.

Sisi ACT-Tanzania tunaofuata misingi ya haki na uwajibikaji tunalaani vikali matendo ya jeshi la polisi kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kukabiliana na viongozi wa kisiasa kama ilivyofanyika jana.

Aina hii ya nguvu ya jeshi la Polisi kwa ajili ya kukilinda chama kilicho madarakani ndiyo iliyopelekea kuuawa kwa mwanahabari Daudi Mwangosi miaka miatatu iliyopita jambao ambalo hatupendi lijirejee kwa mtanzania Mwingine.

Tunalitaka jeshi la Polisi litende haki kwa vyama vyote kwa kuacha uwanja huru wa kufanya siasa, hasa tukizingatia wakati huu wanapowazuia viongozi wa CUF na kuwaruhusu wa CCM kufanya mikutano sehemu mbali mbali nchini kwa njia ya maandamano.

Mwisho tunatoa Pole kwa Prof.Lipumba wanachama n viongozi wote wa Cuf waliokamatwa hapo jana.

ACT TANZANIA TAIFA KWANZA

Imetolewa 
Na Mohmmed Massaga
NAIBU KATIBU MKUU BARA
+255 718 388 888
Tarehe 28/01/2015.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment