Shule Binafsi Zapigwa Stop Na Serikali Kurudisha Wanafunzi Nyumbani Wasiofikia Wastani

Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi, imezipiga marufuku shule binafsi  kuwafukuza au kuwasitishia masomo wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani na kusisitiza kuwa shule zote zitakazokiuka agizo hilo zitachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili.
Agizo hilo limetolewa na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi bungeni, Shukuru Kawambwa mjini Dodoma katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 18 ulianza jana Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu kutokana na swali la msingi la  Conchesta Rwamlaza.
Katika hatua nyingine  Waziri Kawambwa alisema ni marufuku kwa mameneja na wamiliki wa shule binafsi za sekondari kukaririsha, kuhamisha au kuwafukuza shule wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani wa shule husika kwa kuwa kiwango cha ufaulu kilichowekwa na serikali ni wastani wa asilimia 30.
Waziri huyo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Conchesta Rwamlaza (Chadema) ambaye alikuwa anataka kufahamu kama Serikali inafahamu kwamba shule binafsi zimeweka viwango vyao wa alama za ufaulu.
Katika swali lake, Rwamlaza aliongeza kuwa wanafunzi ambao wanashindwa kupata alama zilizowekwa na shule binafsi, wanalazimishwa kukariri darasa au kufukuzwa shule.
Alisema hali hiyo imekuwa inawaathiri wazazi ambao wanapata mzigo wa kuendelea kulipa ada, lakini pia hali hiyo inawapotezea muda wanafunzi hao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment