Murray Afika Fainali 2015 Australian Open

Andy Murray kutoka Uingereza amefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya Australian Open baada ya kumshinda mpinzani wake Tomas Berdych katika mchezo wa hatua ya nusu fainali uliounguruma huko mjini Melbourne.
Murray alionyesha kuwa katika wakati mgumu wa kufikia azma ya ushindi katika mchezo huo, baada ya kufanya vibaya katika seti ya kwanza ya mchezo huo, lakini mpaka mwisho mambo yaligeuka na kumtoa nishai Berdych kwa kumtandisha seti tatu kwa moja ambazo ni 6-7 6-0 6-3 7-5.
Hata hivyo Murray anakua mchezaji wa kwanza kutinga katika hatua ya fainali upande wa wanaume kwa mwaka huu, na sasa anamsubiri mshindi wa mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali utakaochezwa hii leo kati ya Novak Djokovic dhidi ya bingwa mtetezi Stan Wawrinka.
Wakati huo huo mwanadada kutoka nchini Marekani anaeshika namba moja kwa ubora duniani Serena Williams ametinga katika mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya Australian Open baada ya kufanya kazi nzito ya kumshinda mmarekani mwenzake Madison Keys seti mbili kwa sifuri ambazo ni 7-6 na 6-2.
Ushidni huo unamfanya Serena kufika katika hatua ya fainali ya michuano hiyo mara sita na sasa atakutana na Maria Sharapova ambaye alifanikiwa kushinda mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Ekaterina Makarova kutoka nchini Urusi kwa seti mbili kwa sifuri ambazo ni 6-3 6-2.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment