Taasisi ya Mwalimu Nyerere imeandaa Mdahalo kuhusu kuzingatia mambo muhimu katika katiba inayopendekezwa. Huu ni mfululizo wa midahalo na majadiliano kuhusu Katiba inayopendekezwa, mdahalo huo utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 24 /01/ 2015 kuanzia majira ya saa 8:00 mchana mpaka saa 12:00 Jioni katika Ukumbi wa MCC Musoma.
Mdahalo huu unalenga kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu kuzingatia mambo muhimu yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa na kuwapa fursa wananchi kusikiliza mambo ya msingi katika kupiga kura ya maoni kuhusu Katiba.
Ikumbukwe kuwa Taasisi ya Mwalimu Nyerere hailengi wala haikusudii kukosoa au kuanzisha malumbano na mtu wala Taasisi yeyote ile, bali lengo ni kutoa elimu ya uraia na kupanua uelewa wa Katiba inayopendekezwa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment