Mgombea wa mtaa aliyeshindwa wa CCM mtaa wa Mkombozi amefungua kesi mahakama ya wilaya ya Kasulu kupinga ushindi wa chama cha ACT-TANZANIA,ambapo chama cha ACT-TANZANIA kilishinda kwa nafasi ya Mwenyekiti wa mtaa huo.
Uchaguzi uliofanyika tarehe 21/12/2014,madai yake ni kuwa mgombea wa ACT-TANZANIA alipanga njama na msimamizi wa kituo kutangaza matokeo mapema kabla ya muda.
Kesi hiyo kwa mara ya kwanza itatajwa tarehe 02/02/2015.Wakati huo chama Wananchi CUF kimekiburuza mahakamani chama cha NCCR-MAGEUZI kupinga matokeo ya mtaa wa Juhudi,kesi zote zitatajwa tarehe hiyo. Ikumbukwe kuwa mgombea wa ACT-TANZANIA mtaa wa mkombozi alishinda kwa kura 100 kati ya wa CCM aliyepata kura 10.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment