Usher na Kanye West kutingisha BET Awards 2015

Leo ni siku ambayo litarekodiwa tukio la nane la kihistoria la kutunza wanamuziki ambao mchango wao ni mkubwa katika medani ya muziki wa kizazi kipya duniani, maarufu kwa jina la BET Music Awards.
Tukio hili ambalo litaonyeshwa kwa mara ya kwanza Jumatatu kupitia Kituo cha Televisheni cha BET, litawapa heshima wanamuziki ambao wamejidhihirisha kwenye medani ya muziki kibiashara, utashi wao kwenye majukwaa na pia kwa jinsi wanavyoweza kwenda na teknolojia.
Kati ya wanamuziki ambao wametajwa kung’ara katika tukio hilo la aina yake ni pamoja na Kanye West pamoja na Usher Raymond. Hawa kwa pamoja huenda wakatunukiwa kwa mtazamo wao katika muziki na jinsi walivyoigeuza sanaa ya muziki kulingana na wakati.
Usiku huo unaotarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake, pia utanakshiwa na watumbuizaji tisa wanaodaiwa kuwa na mvuto wa jukwaa kwa mwaka mzima wa 2014, huku kwao ikionekana kuwa ni heshima kubwa.
Wanamuziki hao ambao wana rekodi nzuri katika muziki wa kizazi kipya ni pamoja na Mary J. Blige, Ne-Yo, K. Michelle, Trey Songz, Charlie Wilson, Patti LaBelle na Jill Scott.
Ukiachana na Usher na Kanye, Mkuu wa Makumbusho ya Sanaa ya Afrika, Dk Johnnetta B. Cole, atatunukiwa tunzo ya Elimu ya Sanaa kutokana na mchango wake mkubwa kwa wasanii wa kizazi kipya.
Muigizaji, mwimbaji na mtaalamu wa jukwaa, Phylicia Rashad, atatunukiwa tunzo ya juu ya sanaa ya jukwaa. Tunzo ya mwisho itakwenda kwa mwenyekiti wa kampuni ya Microsoft, John W. Thompson, ambaye atatunukiwa tunzo ya biashara na teknolojia ya sanaa.
Tunzo za 2015 kwa mwaka huu, zinarekodiwa leo katika ukumbi wa Warner Theatre huko Washington, DC. huku muongoza shughuli akitajwa kuwa yule yule wa mwaka jana Wayne Brady.
Kung’ara kwa Usher kwenye tunzo za mwaka huu kunatokana na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kwa albam yake My Way. Ile albamu, ilikuwa na nyimbo kama Nice & Slow, My Way na You Make Me Wanna ambazo zilishika chati za juu za Bilboards.
Uwezo mkubwa aliouonesha Usher katika albam hiyo ukasababisha auzo nakala zaidi ya milioni sita.
Albamu ya Usher ya tatu ya R&B iliyoitwa 8701, ilitoka na nyombo mbili kali ambazo ni U Remind Me” na U Got It Bad ambazo kila mtu anajua jinsi zilivyokaa namba moja katika chati mbalimbali.
Albamu iliyokuja na mafanikio makubwa zaidi kwa Usher ni Confessions ya mwaka 2004 ambayo iliuza nakala milioni 20, ikasababisha Usher kuwa mmoja kati ya wasanii waliouza muziki wao kwa kiwango kikubwa katika karne.Mpaka leo, Usher ameshashinda tunzo nane za Grammy. na mwaka 2009, akatajwa kuwa msanii namba moja wa Billboard wa muongo.
Tukija kwa Kanye West, yeye ana rekodi ya kuuza nakala milioni 21 za albamu zake madukani, lakini mtandaoni akiweka rekodi ya kuuza nakala 66,000.
Mwaka 2005, West alitajwa na jarida la Time kuwa ni mmoja kati ya vijana wenye ushawishi mkubwa duniani.
Kanye West ameshashinda jumla ya tunzo 21 za Grammys.
Hizi zaweza kuwa sababu tosha za kwa nini Kanye na Usher wanaweza kutajwa mashujaa wa tunzo hizo kwa upande wa wanamuziki.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment