Halima Mdee Amewalipua Chenge na Idd Simba Kuhusu ATCL, UDA, na PRIDE

Mbunge wa Kawe Halima Mdee amewataja baadhi ya Viongozi katika kashfa mpya ya ATCL, UDA na PRIDE.

Ni katika suala la mikataba mibaya ya wizi wa ATCL, serikali ilkodisha ndege kutoka liberia ambayo ilikuwa imebakiza miezi sita ili ifanyiwe marekebisho makubwa baada ya kutimiza umri w miaka 12.

Serikali ilianza kuilipia hata kabla haijaletwa nchini kuanza kazi husika na ilifanya kazi miezi sita tu, lakini sasa serikali imeendelea kuilipia kwa kiasi cha dola milioni ishirini na tano na inadaiwa bafo kiasi takribani milioni nyingine takriban 25USD.

Waziri wa miundombinu ni yuleyule mzee Chenge na Halima mdee amemtaja live humo bungeni.

Andrew chenge....amehamaki na kusimama akamuomba Halima Mdee atowe ushahidi kama anao, jambo ambalo mdee amesema atalifanya kwa kufuata kanuni za bunge.

Pia kuhusu Idd Simba, Halima mdee amemlipua kwa kuwa nyuma ya Simon group, kampuni ambayo inahusika na kashfa ya UDA na pia kashfa ya uhamishaji wa kampuni ya PRIDE ambayo imehamishwa kinyemela toka serikalini na kumilikishwa kwa Idd simba.

Credit: TBC live 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment