Polisi Moro: Yanga Acheni Visingizio Vyenu

Polisi Morogoro kupitia kwa kocha wao msaidizi, John Tamba imeibeza Yanga inayocheza nayo kesho kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara, kuwa waache visingizio kwa kusema Uwanja wa Jamhuri Morogoro ni mbaya.
Polisi inacheza na Yanga katika uwanja huo ambao umekuwa kero kwa timu za Dar es Salaam hasa watoto hao wa Jangwani na Simba, ambazo pia imekuwa ni kama kawaida yao kupata matokeo mabaya hapo.
Tamba alisema imekuwa kama kawaida kwa makocha wa timu hiyo na nyingine za Dar es Salaam kusema Uwanja wa Jamhuri si mzuri, wakati vile wanavyovitumia wao kwa mazoezi havifai.
“Nawashangaa sana, nimesikia Yanga wanalalamikia uwanja hivi huu na ule wa Loyola upi mzuri,” alihoji Tamba na kuongeza.
“Waache visingizio, Uwanja wa Jamhuri ni mzuri na ndiyo maana TFF wameupitisha, pia mbona wao wanafanya mazoezi kwenye viwanja vibovu kabisa kama kile cha Loyola.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment