Watu wanne wauawa kwenye maandamano nchini Kongo.
Watu wanne walipoteza maisha akiwemo askari wawili kwenye mji mkuu wa Kongo Kinshasa baada ya polisi kutumia nguvu kuwatawanya mamia ya watu wanaopinga Rais Joseph Kabila kuongeza muda wa kukaa madarakani.
Na zaidi ya watu 10 walijeruhiwa kwenye maandamano hayo baada ya polisi kutumia silaha za moto kuwadhibiti waandamanaji hao kwenye maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo hapo jana.
Pia polisi walitumia mabomu ya machozi kutawanya makundi ya vijana ambao walikuwa wanachoma magurudumu ya magari barabarani.
Msemaji wa serikali Lambert Mende amesema kuwa askari hao wawili waliuawa kwa risasi.
0 comments:
Post a Comment