Wapiga kura nchini Zambia wanaelekea kwenye vituo vya kupiga kura katika uchaguzi wa urais uliosababishwa na kifo cha Michael Sata mwaka uliopita.
Uchaguzi unatarajiwa kuwa na mchuano mkali baina ya Edgar Lungu kutoka chama tawala na Patriotic Front na Hakainde Hichilema kutoka chama cha United Party for National Development.
Mtangazaji Nomsa Maseko wa BBC aliyepo mjini Lusaka amesema wagombea wote wameahidi kukuza mfumo wa elimu na kuunda ajira.
Mshindi atatumikia muda wa miezi 18 ya kipindi cha Michael Sata.
Zambia inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu mwaka 2016.
Credit: BBC
0 comments:
Post a Comment