Msanii wa muziki nchini Fid q |
Msanii nguli wa Bongo Fleva, Farid Kubanda ‘Fid Q’, amesema wakati umefika kwa serikali kutambua muziki ni ajira kwa vijana wengi nchini.
Akizungumza kutoka jijini Dar es Salaam, Fid Q amesema serikali inapaswa kuziunga mkono jitihada za wasanii wa bongo fleva kwa kupambana vikali na maharamia wa kazi zao.
“Ikumbukwe sanaa ya muziki ni kazi kama zilivyokuwa kazi zingine , Serikali ina kila sababu ya kuwaunga mkono wasanii wa tasnia hiyo,” alisema Fid Q.
Aliendelea kusema kuwa kwa kufanya hivyo kutawawezesha wasanii kunufaika na kazi zao.
0 comments:
Post a Comment