Kapteni John Damiano Komba, alilitumikia Taifa na Chama chake katika ngazi nyingi, kama Askari wa Jeshi la Wananchi ambako wengi ndipo tulipomfahamu kutokana na umahiri wake katika Utunzi na Uimbaji wa Nyimbo za Kwaya!
Kabla ya kifo chake, Kapteni Komba pia alikuwa kiungo cha muhimu katika uanzishwaji wa Tanzania One Theatre, kama sehemu ya shughuli za Uenezi za Chama Cha Mapinduzi, na huko tulishuhudia wakivuna kwa mahadhi tofauti kuanzia Kwaya, Maigizo, Ngoma za Asili, Taarabu na Muziki wa Dansi.
Kapteni Komba pia atakumbukwa kwa nyimbo alizotunga za kumuaga na kumuenzi Marehemu Mwalimu Nyerere, maara baada ya kupokea taarifa za msiba huo mkubwa katika historia ya Tanzania. Marehamu aliwatumikia wananchi wa Mbinga Magharibi tangu mwaka 2005 hadi umauti ulipomkumba.
Video ya Msemaji Mkuu Mkuu wa CCM akisema neno juu ya Kifo cha Kapten John Damiano Komba
0 comments:
Post a Comment