Hii Ndio Orodha ya Wachezaji Wenye Umri Mdogo Watakaocheza AFCON 2015


Mashindano ya AFCON 2015 yakiwa karibu kuanza kuna wachezaji wenye umri mdogo ambao wataonekana kwenye fainali hizi nao ni;
Nabil Bentaleb (Algeria)
Ni mzaliwa wa Algeria ana umri wa miaka 20  anacheza nafasi ya kiungo wa kati kwenye klabu ya Uingereza Tottenham.
Huyu mchezaji iliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Algeria.

Rivaldo Coetzee (Afrika Kusini)
Mchezaji huyu nchini kwao anaitwa Rivaldo kutokana na ufungaji wake wa magoli huku akifananishwa na nyota wa Kibrazil Rivaldo.
Rivaldo anacheza nafasi ya kiungo wakati kwenye timu yake ya taifa Bafana Bafana.
Kwasasa anachezea klabu ya Ajax Cape Town.
François Kamano (Guinea)
Mchezaji huyu alizaliwa  mwezi wa tano mwaka 1996 ni mshambuliaji wa klabu ya SC Bastia ya Ufaransa.
Francois ana umri wa kiaka 18 na alisaini mkataba wa miaka minne katika klabu hiyo.
 Ronald Kampamba (Zambia)
Mchezaji huyu ana umri wa miaka 20 ni mshambuliaji wa klabu ya Nkana Zambia.
Ronald msimu wa 2012-13 alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Zambia akiwa na magoli 18 na kuisaidia klabu yake kubeba kombe.
 Fabrice Ondoa (Cameroon)
Mchezaji huyu alizaliwa mwaka 1995 na ni mlinda mlango wa timu ya taifa ya Kameruni.
Eric Bertrand Bailly (Ivory Coast)
Mchezaji huyu ana umri wa miaka 20 anacheza nafasi ya kiungo wa kati katika klabu ya espanyola
N’Tji Michel Samake (Mali)
Ni mlinda mlango mwenye umri wa miaka 20 yuko kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya mali ambao wanaelekea guinea ya ikweta katika fainali za AFCON.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment