Chris Brown akifuatilia mwenendo wa kesi hiyo, katika mahakama ya Los Angeles Superior Court |
Jaji wa mahakama ya Los Angeles Superior Court, James Brandlin, amekataa ombi lililotolewa na mwanasheria Mark Gregory kukiondoa kipengele cha kumweka chini ya uwangalizi wa kisheria mteja wake Chris Brown 24,
katika kesi inayomuandama mkalii huyo wa R&B tangu mwaka 2009 baada ya kumpiga Rihhana aliyekuwa mpenzi wake.
Maamuzi hayo Jaji yamekuja mara baada ya Chris Brown kukiuka masharti ya baadhi ya vipengele vya adhabu alivyokuwa amewekewa na mahakama hiyo,
ikiwa ni pamoja na kutomaliza kwa wakati adhabu ya kufanya kazi za kijamii alizopewa muda wa saa 1000
Mwanasheria Mark Gregory, akitoa utetezi kwa niaba ya mteja wake |
lakini mpaka sasa amebakiza muda wa saa 200 anazotakiwa kuzimaliza mwisho wa mwezi Januari,
kosa lingine alilofanya ni kusafiri na kwenda kufanya ‘Show’ njee ya County ya Los Angeles bila kuwa na vibali kutoka katika mahakama ya Los Angeles.
Katika upande wa utetezi mwanasheria, Mark Gregory, alidaikuwa mteja wake alifanya kosa hilo kufatia ushauri mbaya uliotolewa na ofisi yake.
juu ya kutokuepo kwa ulazima wa kuomba kibali cha kusafiri njee ya County ya Los Angeles.
Hata hivyo Jaji wa mahakama hiyo ameamua kumwachia huru Chris Brown mpaka tarehe 20 ya mwezi Machi mara baada ya ripoti ya uchunguzi kukamilika.
0 comments:
Post a Comment