TRA yakamata mifuko 40 ya sukari na vigae

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kupitia idara ya forodha, imekamata mali ya magendo iliyokuwa iliingizwa nchini kwa njia hisiyo halali kupitia bandari bubu ya kunduchi, jijini dar es salaam.
Naibu kamishna wa forodha, Patrick kisaka, ametaja mali hizo kuwa ni mifuko 40 ya sukari kutoka brazil, ndoo 20 za mafuta ya kupikia kutoka mashariki ya mbali na katoni 70 za vigae.
Kisaka aliwahakikishia wananchin kuwa idara yake ikishirikiana na askari wa doria wataendelea kupambana na wafanyibiashara wa magendo katika maeneo ya mjini na nchi kavu usiku na mchana ili kuhakikisha serikali inapata mapato yake, ambayo imekuwa ikipotea kwa njia hizo za kimagendo.
Katika kipindi kisicho zidi mwaka Mmoja mamlaka ya kupitia idara hiyo imeshakamata zaidi ya mifuko elfu moja 1,158 ya sukari ya kilo 50 kutoka nje ya nchi Iliyoingia nchini kimagendo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment