Mwili huo utaagwa kuanzia saa nne asubuhi kabla ya kusafirishwa kwenda Mbinga kwa maziko siku ya Jumanne.
Kifo cha Marehemu Komba kinakuwa ni pigo jingine kubwa katika tasnia ya Burudani kutokana na mchango wake, na kwa niaba ya wadau wengine wa tasnia hiyo, tumeongea na Asha Baraka kutoka msibani, ambaye ameeleza kuwa Kapteni Komba ni mfano wa kuigwa na wasanii Wengine kutokana na kujituma kwake katika sanaa, akiwa pia na mchango mkubwa katika kukitangaza chama cha mapinduzi kupitia sanaa yake hiyo.
Marehemu Kapteni Mstaafu John Komba alifariki dunia jana kwa tatizo la shinikizo la damu katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala pema peponi Amina.
0 comments:
Post a Comment