69 Wafa kwa Kunywa Pombe Yenye Sumu

Idadi ya watu waliokufa baada ya kunywa pombe yenye sumu iliyotengenezwa nyumbani nchini Msumbiji imefikia 69, imeripoti redio ya nchi hiyo.
Bia hiyo, kawaida hutengenezwa kwa mtama, huenda ilichanganywa na magamba ya mamba, afisa afya alieleza.
Mtoto mdogo alikuwa miongoni mwa waliokufa baada ya kunywa pombe hiyo kwenye msiba kwenye jimbo la Tete siku ya Jumamosi.
Afisa huyo alisema ilikuwa lilikuwa pigo kubwa kuikumba Msumbiji, huku watu 39 wakiendelea kutibiwa hospitali.
Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo katika agizo lilitolewa Jumapili.
Bia hiyo, inayojulikana kama “phombe”, kimili hutumiwa kwenye shughuli za jimbo la Tete nchini Msumbiji.
Vifo kutokana na unywaji wake ni nadra, waandishi wanasema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment