Bendi ya muziki wa dansi ya Sikinde, imeahidiwa kununuliwa vyombo iweze kuendeleza ushindani na kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki wake.
Ahadi hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Temeke jijini Dar es Salaam, Abbas Mtemvu.
Mbunge huyo alizialika bendi kongwe za Sikinde na Msondo Ngoma katika hafla ya kuwapongeza Wenyeviti wa Serikali za mitaa.
“Naahidi nitajitahidi kuwatafutia ala za muziki bendi ya Sikinde, iweze kutoa burudani katika kiwango bora zaidi,” alisema Mvtemvu.
Kwa muda mrefu, Sikinde imekuwa na kilio cha kuhitaji vyombo vya muziki, kufuatia vilivyopo kuonekana kuchoka.
0 comments:
Post a Comment