Breaking News: Sakata la Escrow Lawapandisha Kizimbani Vigogo Watatu Kutoka Tanesco, TRA na BOT..

Vigogo watatu kutoka katika taasisi tatu nyeti za Serikali wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakituhumiwa kuhusika katika sakata la uchotwaji wa mabilioni ya fedha kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Vigogo waliofikishwa mahakamani hapo leo, kutoka Benki Kuu Tanzania (BoT) Steven Urassa, Shirika la umeme (Tanesco) Kyabukoba Rutabingwa, na kutoka Mamlaka ya Mapato ( TRA) ni Julius Angelo ambaye amekosa dhamana.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imeitupia zigo ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ili kuchukua hatua ya kuwafikisha mahakamani vigogo wote wakiwamo mawaziri.


Pamoja na wengine watakaobainika kwenye uchunguzi wake nakukutwa na hatia ya kuhusika na vitendo vya rushwa katika sakata la uchotwaji wa sh202bilioni katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment