Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm anafikiria kufumua kikosi chake kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
Pluijm alimwambia Mwandishi Wetu jijini Dar es Salaam jana kuwa amefikia hatua hiyo kuhakikisha timu yake inapata ushindi katika mechi hiyo na zingine zinazofuata.
“Nafumua kikosi changu baada ya kutolewa kwenye kombe la Mapinduzi nimegundua mambo kadhaa yanahitaji kufanyiwa kazi.
“Moja kati ya mambo hayo ni kubadili kikosi kwa kufanya hivi ushindi unaweza kupatikana,” alisema Mholanzi huyo.
0 comments:
Post a Comment