Tff Yatoa Ratiba Mpya ya Ligi Kuu Bara

Vituko vya TFF!!!! Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa ratiba mpya ya Ligi Kuu ikionyesha leo Yanga wananacheza na Coastal Union leo Uwanja wa Mkwakwani Tanga na Azam FC na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba Bukoba.

Lakini ajabu timu zote Yanga na Azam hazina taarifa na mechi hizo na zote hazipo kwenye vituo vya michezo hiyo.
Meneja wa Azam FC Jemedari Said amesema wapo mkoani Shinyanga na wanajua mechi yao ni mwishoni mwa wiki.
Kwa upande wake, Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh amesema timu yao ipo kambini Bagamoyo inajiandaa na mechi na Ruvu Shooting Jumamosi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment