Maisha ya Marehemu TX Moshi kutengenezewa Makala

Hassan TX Moshi Junior
Kutoka bendi ya Msondo Ngoma, Baba ya Muziki Tanzania msanii Hassan TX Moshi Junior, ameweka wazi ujio wa Makala maalum itakayohusu maisha ya Marehemu Baba yake, aliyekuwa msanii mahiri wa muziki wa Dansi hapa nchini.
Marehemu TX Moshi Enzi za Uhai Wake

TX Moshi Junior ambaye anafanya vizuri kwa upande wa uigizaji filamu pia amesema kuwa, Makala hii mbali na kuonesha maisha ya baba yake aliyefariki takriban miaka 9 iliyopita, pia kwa sehemu itaonesha safari yake binafsi katika kuingia kwenye muziki huo.
TX Moshi Junior amesema kuwa, kazi ya kuanza kuitengeneza makala hii itaanza mapema mwishoni mwa mwezi huu, na inatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi kifupi baada ya hapo, na pia inatarajiwa kutoka na baadhi ya kazi za filamu kutoka kwake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment