Tamasha la Kiboko Yao Kutikisa Dar Jan 24

Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Mwa Fa (Katikati), ambae ni moja ya wasanii watakaotumbuiza katika onyesho la Tigo Kiboko Yao Music Concert tarehe 24 mwezi huu  Leaders Club .

Kampuni ya simu ya mkononi ya tiGO imetangaza kuandaa tamasha kubwa kabisa la muziki la aina yake lijulikanalo kama “Kiboko Yao” litakalofanyika Januari 24, mwaka huu Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni.



Akiongea leo katika mkutano wake na waandishi wa habari Meneja wa Chapa wa tiGO William Mpinga, amesema tamasha hilo litatumbuizwa na wasanii 18 wakali, linaenda sambamba na kutambulisha huduma mpya ya tiGO Music itakayowaletea wateja wao burudani ya muziki kupitia simu zao.
Katika Mkutano huo na waandishi wa habari pia walikuwemo baadhi ya wasanii watakaopanda jukwaani katika tamasha la Kiboko Yao, akiwemo Diamond Platnumz, Ali Kiba, Christian Bella, Ben Pol, Mwana FA, Fid Q, Isha Mashauzi, Vanessa Mdee, Yamoto Band pamoja na bendi kongwe za Msondo na Sikinde.


Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia matangazo yetu ya SbmTv, Radio, Blogu www.http://sbmbroadcast.blogspot.com pamoja na ukurasa wetu wa facebook SbmTv https://www.facebook.com/pages/Sbm-Tv/1547129342201781 kila wakati.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment