Falcao Anaweza Kuondoka Man U

Mshambuliaji wa Manchester United Radamel Falcao anaweza asiwepo Old Trafford msimu ujao, ameeleza wakala wake.
Raia wa Colombia, ambaye analipwa pauni 265,000 kwa wiki, amefunga magoli matatu katika mechi 13 tangu asaini kutoka Monaco kwa mkopo wa msimu mmoja kwa pauni milioni sita mwezi Septemba.
United watakuwa naye hadi Mei ili kumnunua kwa ada ya pauni milioni 40.
“Atacheza katika moja ya vilabu bora duniani msimu ujao, huenda ikawa Man United au isiwe, alisema wakala wa Falcao 28, Jorge Mendes.
Maisha ya soka ya Falcao katika dimba la Old Trafford yameathiriwa na majeraha ya kigimbi cha mguu na ameanza kwenye mechi nane tu.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment